• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Itunzeni Mitaro ya Maji- RC Kafulila

Posted on: February 19th, 2022

ITUNZENI MITARO YA MAJI-RC KAFULILA.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu,David Kafulila amewataka wananchi wa Mji wa Maswa mkoani humo kuitunza Mitaro ya maji ya mvua inayojengwa kwenye baadhi ya barabara za mitaa ya mji huo.

Sambamba na kuitunza amewataka kuifanyia usafi wa mara kwa mara na kutotupa takataka ndani ya mitaro hiyo ili iweze kuwasaidia kusafirisha maji ambayo awali yalikuwa wakiingia kwenye nyumba zao hasa nyakati za mvua.

Mkuu huyo wa mkoa amesema haya mara baada ya kutembelea ujenzi wa mitaro yenye urefu wa kilomita 5.5 inayojengwa kwenye mji huo chini ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini(TARURA).

Kafulila ambaye ameridhishwa na ujenzi huo unaoendelea amewataka Wakandarasi wote waliopewa kazi hiyo kukamilisha kwa wakati kama mikataba yao waliyosaini na TARURA, Simiyu kwani Serikali imetoa fedha hizo kupitia tozo za mafuta na mfuko wa barabara.

Naye Meneja wa Tarura wilaya ya Maswa,Mhandisi David Msechu amesema kuwa wanatekeleza miradi mitano ya ujenzi wa mitaro hiyo yenye thamani ya Sh 532,936,640.Amesema mradi huo unatekelezwa kupitia kampuni mbalimbali ambazo ni pamoja na Kampuni ya MMETO CONSTRUCTION CO LTD ya Dar Es Salaam kwa gharama ya Sh Milioni 100,Kampuni ya FRESAM CONSTRUCTION CO LTD ya Mwanza kwa gharama ya Sh Milionib111.2 na Kampuni ya ASSA GENERAL SUPPLIERS AND CONSTRUCTION CO LTD ya Bunda,Mara kwa gharama ya Sh Milioni 69.

Kampuni nyingine ni MORAJ WOMEN GROUP ya Shinyanga kwa gharama ya Sh Milioni 200 na Kampuni ya WAMAMA KAZI ya Tukuyu,Mbeya kwa gharama ya Sh Milioni 52.6

Mhandisi Msechu amesema katika kutekeleza mradi huo, mradi huo unakabiliwa na changamoto ya kuwepo kwa miundo mbinu ya maji iliyokatisha au kupita sambamba na barabara ambayo imesimikwa kina kifupi kukatwa na kusababisha baadhi ya wananchi kukosa huduma ya maji ila wamekuwa wakishirikiana na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Maswa (Mauwasa)kuirejesha kwa wakati ili wananchi wapate huduma ya maji.Mwisho

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa