• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

IGP SIRRO:Makamanda wa Polisi Mikoa Watabaki Kwenye Vituo Vyao Uhalifu Ukipungua

Posted on: July 26th, 2017

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Inspekta Generali Simon Sirro amesema Makamanda wa Polisi wa Mikoa wataendelea kubaki katika vituo vyao vya kazi endapo watatimiza wajibu wao na kupunguza uhalifu katika mikoa yao.

IGP Sirro ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu katika mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kamaliza mazungumzo yake na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa yaliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

IGP Sirro amesema Makamanda wa Polisi Mikoa wanapaswa kutimiza wajibu wao  katika kujali na kusimamia suala la Ulinzi na Usalama katika mikoa yao ili wananchi wakae kwa amani na mali zao ziwe salama.

“ Moja ya lengo la ziara yangu ni kuwakumbusha askari wa jeshi la polisi uwajibikaji na kuwajibika ni pamoja na kulinda watu na mali zao,  makamanda wa polisi mikoa nimewaambia kamanda ataendelea kukaa kwenye mkoa ule kama uhalifu utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa” amesema Sirro

Inspekta Sirro amesema ziara yake pia imelenga kuwakumbusha askari majukumu yao katika kuhakikisha wanawajibika kutimiza kiapo chao na kutenda haki ili wananchi waendelee kuliamini Jeshi la Polisi.

Kiongozi huyo pia ameelekeza viongozi wa jeshi la polisi wasiwanyime haki ya  dhamana watu wenye makosa ya kawaida ambayo yana  dhamana isipokuwa kwa makosa makubwa yakiwepo ya mauaji, kughushi na mengine yanayohitaji upelelezi.

Kuhusu suala la kuwepo kwa mahusiano mabaya kati ya baadhi ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Waandishi wa habari, Inspekta Sirro amefafanua kuwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa watimize wajibu wao kama watumishi wa Umma kwa kuwajali waandishi kama wanavyowajali wateja wengine kwa kufuata sheria na akawataka waandishi wa habari wafuate sheria, kanuni na taratibu pasipo kuvuka mipaka.

Akakimkaribisha Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini, katika Mkoa wa Simiyu Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka amemshukuru Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Boniventure Mshongi na Jeshi la Polisi kwa ujumla kwa namna wanavyoshirikiana katika suala la ulinzi na usalama.

Aidha, amemuomba Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini kuona uwezekano wa kusaidia kujenga majengo ya Ofisi na nyumba za makazi kwa ajili ya  Askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo.

Inspekta Simon Sirro amewasili Mkoani Simiyu akitokea Mkoani Mara akiwa katika ziara yake ya kikazi ambapo pamoja na kuzungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, Wakuu wa Wilaya ambao pni Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya,  pia  amezungumza na viongozi na askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa