• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Hatutawaweka Karantini Wasafiri wa Ndani ya Nchi: RC Mtaka

Posted on: April 17th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema  Simiyu itaendelea kufuata  maelekezo ya Serikali katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona, ikiwa ni pamoja na kuwatowaweka  karantini wasafiri wanaotoka katika mikoa yenye maambukizi kama inavyopendekezwa na baadhi ya wananchi badala yake itawaweka wasafiri kutoka nje ya nchi.

Mtaka ameyasema hayo leo Aprili 17, 2020  wakati wa uhamasishaji wa zoezi endelevu la upuliziaji dawa kwenye magari ya abiria katika kituo kikuu cha mabasi Bariadi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona, ambalo limeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

“Tumeona kauli za viongozi mbalimbali, tumeona pia jumbe za watu wa Simiyu katika mitandao mbalimbali ya kijaamii ambao wangetamani watu kutoka katika mikoa yenye maambukizi wawekwe karantini sisi kama mkoa tunasema hapana,  maelekezo yote kuhusu Corona yanatoka kwa Mhe. Waziri Mkuu na mpaka sasa wasafiri wanaowekwa karantini ni wanaotoka nje ya nchi,” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka ametoa  wito kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya na kutoa taarifa kwa wataalam wa afya pale wanapohisi kuwa na dalili zinazotajwa kwa mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Corona ili waweze kupata msaada stahiki wa kitaalam.

“Watu walioko karantini hawajasakwa na polisi tunao watu wanaotoka safari za mbali na kuja kuomba wenyewe watengwe, wengine familia zao zinaleta taarifa  kuwa zina mgeni wa aina fulani na kuomba ajitenge, jamii zetu zimekuwa na uelewa wa kutosha kwani zinapoona mgeni zinatoa taarifa kwenye mamlaka husika nayo inachukua hatua,”alisema Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka amesisitiza kuwa  zoezi endelevu la upuliziaji dawa kwenye magari ya abiria lifanyike mapema bila kuathiri ratiba za wasafiri huku akiwataka makondakta kuhakikisha wanawasimia abiria wamenawa mikono yao kwa kutumia kwa kutumia maji yenye dawa . maji tiririka na sabuni na ambao wana vitakasa mikono wavitumie.

Mtaka amebainisha kuwa mpaka sasa Mkoa hauna mgonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya Corona na kuongeza kuwa ni vema wananchi watumie siku tatu kuanzia leo Aprili 17, 2020 hadi 19 Aprili, 2020 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kumuomba Mwenyezi Mungu ili aweze kutuepusha na janga hili.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt.Festo Dugange amesema hadi sasa jumla ya watu 120 kutoka nje ya nchi wamewekwa kwenye maeneo ya uangalizi maalum (karantini) katika mabweni ya shule za sekondari, ambapo watu 18 kati yao wameruhusiwa baada ya kumaliza siku 14 na kugundulika kuwa hawana maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa homa ya mapafu (Corona COVID-19).

Kwa upande wake Kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Henry Mwaibambe amewataka wananchi wa Mkoa huo kufuata maelekezo yaliyotolewa na serikali huku akiongeza kuwa jeshi hilo halitosita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yeyote ambaye atakiuka au kushindwa kufuata maelekezo.

Nelson Rambo ni kondakta wa basi la Kwangus Express linalofanya safari zake Bariadi -Mwanza amesema kuwa wanafuata maelekezo yaliyotolewa na serikali kwa abiria wanaopandia njiani kunawa mikono pamoja na kupuliza madawa kwenye mabasi.

Akizungumza kwa niaba ya abiria Rehema Mapalala ameishukuru serikali kwa zoezi hilo la upuliziaji wa madawa kwenye mabasi na kusema kuwa wamelipokea kwa furaha kwani linajali afya za wasafiri huku akiomba elimu iendelee kutolewa kwani siyo wananchi wote waliopata elimu ya namna ya kujikinga na virusi vya Corona.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/04/hatutaweka-karantini-wasafiri-wa-ndani.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa