• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Halmashauri ya Maswa yatoa Milioni 50 kwa Vijana na Wanawake

Posted on: November 1st, 2017

Jumla ya vikundi 16 vya wanawake na vijana vilivyopo katika kata 36 Wilayani Maswa Mkoani Simiyu vimepatiwa mkopo wa shilingi Milioni 50 kwa ajiri ya kuboresha kilimo cha pamba katika maeneo yao.

Vikundi hivyo ambavyo hujishughulisha na kilimo cha pamba vimepokea hundi hiyo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018.

Akizindua msimu wa kilimo na kukabidhi hundi kwa vikundi hivyo Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt Seif Shekalage alisema halmashauri imetekeleza sera ya kuwawezesha vijana na wanawake kwa kuwajengea uwezo katika kujiletea maendeleo ya kujikomboa na umaskini.

Alisema halmashauri imefanikiwa kutekeleza sera hiyo ya kutoa asilimia 5 kwa wanawake na 5 kwa vijana ili kuhakikisha wanajenga uchumi na kipato cha kila mwananchi wa Wilaya hiyo.

Dk Shekalage aliongeza kuwa akinamama na vijana wanapaswa kutambua matumizi sahihi na makusudio ya mkopo waliopokea ili uweze kuwanufaisha katika shughuli zao za kilimo.

Aidha kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa Roggers Limo alisema kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita 2013/2014 hadi 2016/2017 Wilaya yao ilitoa mkopo wa kiasi cha shilingi Mil 75,955,000 kwa vikundi vya wanawake na shilingi 105,182,500 kwa vikundi vya vijana ambapo Milioni 30,162 ,500 ni mapato ya ndani ya Halmashauri.

Hata hivyo Afisa kilimo wa Wilaya hiyo Christopher Simwimba alivitaka vikundi hivyo kutumia mkopo huo ipasavyo na kuhakikisha kabla ya kuanza kupanda katika mashamba yao ni lazima waondoe mazalia ya pamba yaliyokuwa yamebaki ili yasije kuharibu pamba mpya itakayopandwa.

Simwimbi pia aliwasihi wakulima hao kupitia vikundi vyao kutumia mbolea ya samadi ili kurutubisha udongo wa mashamba yao sambamba na kupanda kitaalamu wa kuzingatia sentimeta 90 hadi 40 kwa kila mstari .

Nao baadhi wa wanakikundi vya vikundi hivyo wameishukuru Halmashauri hiyo kwa jitihada wanazozifanya za kuhakikisha wanainua na kufufua kilimo cha zao la pamba ambalo limeonekana kushuka kwa kiwango cha uzalishaji.

Haji Mwarabu mwanakikundi kutoka katika kikundi cha Huruma katika kata ya Mataba aliihakikishia Halmashauri hiyo kupitia Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri yao Dkt Fredrick Sagamiko kuwa watautumia vizuri mkopo huo ili waweze kubadilisha maisha yao kupitia kilimo cha pamba.

Baadhi ya wanavikundi vya vijana na wanawake Wilayani Maswa ,watendaji wa Halmashauri na Baadhi ya madiwani wakiwa katika uzinduzi wa msimu wa Kilimo mwaka 2017/2018 na utoaji wa hundi ya shilingi Milioni 50 kwa vikundi vya wanawake na vijana .

Mkuu wa Wilaya ya Maswa Maswa Dkt Seif Shekalage akimkabidhi mbegu za pamba aina ya YKM08 mwanakikundi cha mama na mtoto ni familia kutoka katika kata ya Kadeto Veronica Seloli wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimowilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa Maswa Dkt Seif Shekalage (KATIKATI) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mhe.Lucas Mwaniyuki ,pamoja na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya maswa mara baada ya makabidhiano ya hundi ya Milioni 50 kwa vikundi 16 vya wanawake na vijana vinavyojihusisha na kilimo.


Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa