• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

DPP Awasimamisha Kazi Mawakili Wawili wa Serikali Simiyu

Posted on: July 11th, 2020

Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka nchini (DPP),  Bw. Biswalo Mganga amewasimamisha kufanya kazi za mashtaka mawakili wa Serikali mkoani Simiyu, Amani Kirua na Twahab Yahaya kwa tuhuma za kuwaachia huru watuhumiwa saba wa mauaji ya bibi kikongwe Nchambi Sing’hini  mkazi wa kijiji cha Kinamwigulu wilayani Maswa kinyume na taratibu.

DPP ameyasema hayo Julai 10, 2020 mjini Bariadi wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo pia amemuagiza naibu mkurugenzi wa mashitaka kuwachukulia hatua za kinidhamu haraka; huku akibainisha kuwa mawakili hao hawataenda mahakamani wala kupewa majalada ya mashtaka wakati taratibu za kinidhamu zikiendelea.

“Kuanzia leo mawakili hawa nimewasimamisha kufanya kazi za mashtaka yaani hawataenda mahakamani wala hawatapewa jalada lolote,wakati taratibu za kinidhamu zikiendelea, wakati huo huo jeshi la polisi liendelee kuchunguza kujua ukweli juu ya ‘involvement’ (ushiriki) yao, nkama kuna rushwa na mambo mengine yoyote yamefanyika,” alisema DPP Mganga.

Aidha, DPP Mganga amesema  yapo maelekezo yanayopaswa kufuatwa na mawakili kabla ya  kufuta kesi ambayo ni pamoja na kuandika kwenye jalada sababu zilizofanya kesi ifutwe na mkuu wa mashtaka katika eneo husika kutoa kibali cha kesi kufutwa, ambayo yote yalionekana kutozingatiwa katika ufutaji wa kesi hiyo.

Katika hatua nyingine DPP Mganga amelitaka jeshi la polisi liendelee kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji walioachiwa kinyume na taratibu na liwarejeshe mahakamani huku akibainisha kuwa jeshi hilo limeshawakamata watuhumiwa wawili ambao hakuwataja majina kwa sababu za kiupelelezi na watapelekwa mahakamani Julai 13, 2020.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga amesema serikali haitawavumilia watumishi wa umma wanaokiuka taratibu kwa maslahi yao binafsi hivyo itaendelea kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.

Aidha,  Mmbaga ametoa wito kwa wananchi kuwa na imani na serikali yao na vyombo vyake kwa kuwa mifumo ya serikali ipo na inafanya kazi huku akiwataka kuwa huru kutoa taarifa wakati wowote kupitia vyombo vya ulinzi na usalama.

Mawakili wawili wa Serikali waliosimamishwa kufanya kazi za mashtaka mkoani Simiyu wanatuhumiwa kuwafutia watuhumiwa saba kesi ya mauaji namba moja ya mwaka 2019 ya mauaji ya bibi kikongwe Nchambi Sing’hini,  ambapo alibainika kuwa watuhumiwa wawili walifutiwa kesi hiyo Desemba  31, 2019 na wakili Twahab Yahaya na watano walifutiwa kesi hiyo Juni 17 mwaka huu na wakili Amani Kirua kinyume cha taratibu.

MWISHO

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa