• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Dkt Bashiru ashauri Wakuu wa Mikoa Kujifunza Simiyu

Posted on: January 5th, 2019

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.

Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.

Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa namna wanavyoshirikiana na viongozi wa Chama kwa namna wanavyosimamia shughuli za maendeleo.

“Niwapongeze  kwa namna mnavyosimamia shughuli za maendeleo, nilikuwa hapa mwaka 2005 kama msimamizi wa uchaguzi nilizunguka maeneo mengi mengine yalikuwa hayapitiki, leo nimekuja nikazungushwa maeneo machache tu, nimeona mambo mengi sana ya tofauti kwa hiyo uongozi wa mkoa huu kwa Chama na Serikali umefanya kazi kubwa na bado mna nafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa zaidi” alisema

Aidha, amesema ili uchumi uwe imara, wa kisasa na wenye manufaa ni lazima uwe jumuishi na uwalenge watu walio wengi ambao ni wazalishaji wadogo hususani katika  katika sekta ya kilimo na viwanda huku akisisitiza umakini zaidi ili uwepo wa viwanda na maendeleo ya kilimo viwanufaishe wengi.

Ameongeza kuwa wakati Mkoa wa Simiyu unapanga mipango mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi ni vema kukawa na mpango wa matumizi bora ya ardhi, ili kuondoa migogoro kwa watumiaji ambayo inakuwa chanzo cha chuki na watu kuishi kwa wasiwasi.

Katika hatua nyingine Dkt. Bashiru amesema CCM imejipanga kuhakikisha kuwa itasimamia na kuimarisha ushirika ambao utasimamiwa na wataalam wenye taaluma na maadili ili uweze kuwanufaisha wanaushirika na kutatua changamoto zao.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa Viongozi na watendaji wa Serikali Mkoani humo watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM huku akisisitiza kuwa fedha zote zinazoletwa katika mkoa wa Simiyu zitasimamiwa vizuri na zitafanya kazi iliyokusudiwa.

Aidha, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unafanya utafiti kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) ili kubaini fursa za kiuchumi zilizopo katika katika kila kijiji kwa Vijiji vyote 470, ambapo utekelezaji wa Falsafa ya Kijiji Kimoja Bidhaa Moja(OVOP) unatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi Februari.

Ameongeza kuwa viwanda vikubwa vitatu vyenye uwezo wa kuajiri takribani wafanyakazi 2000 kikiwepo kiwanda cha chaki na kiwanda cha vifungashio (Maswa) kiwanda cha bidhaa 18 za afya  zitokanazo na pamba(Bariadi)  vitajengwa mwaka huu  2019 Simiyu.

“Ndugu Katibu Mkuu mwaka jana wakati Mhe. Rais anapokea ndege ya Air Bus alicheza muziki na  ukiangalia ilikuwa ni kitu kinachotoka moyoni kuonesha furaha yake, ninaamini mwaka 2019 Mhe. Rais ataucheza muziki huo hapa Simiyu” alisema Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu amesisitiza viongozi na wanachama kuimarisha uhusiano mzuri, kusaidiana na kupendana katika maisha ya siasa huku akiwasihi viongozi kulinda na kuheshimu dhamana walizopewa kwa kutimiza wajibu wao.

Akitoa salamu kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu, Mbunge wa Bariadi,Mhe. Andrew Chenge ametoa wito kwa viongozi na wanachama wa CCM mkoani Simiyu kudumisha upendo, umoja na mshikamano hususani katika kipindi cha kueleka uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally yuko Mkoani Simiyu kuanzia Januari 05,2019 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani humo.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/01/dkt-bashiru-ashauri-wakuu-wa-mikoa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa