Kaimu Kamishna wa Fedha na Logistiki wa Jeshi la Polisi ambaye pia ni mlezi wa mikoa ya Kipolisi ya Simiyu, Geita, Kagera, Mara, Mwanza na Tarime, Dhahiri Kidavashari amefanya ziara leo Agosti 26, 2020 mkoani Simiyu.
Katika ziara yake amekutana na viongozi na askari wa Jeshi la polisi Viongozi wa Mkoa ambapo ziara yake ililenga kuangalia utayari wa askari wa jeshi la Polisi kuelekea katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.
"Sisi kama Jeshi la Polisi tumejipanga katika kuhakikisha kwamba amani na utulivu unatawala katika kipindi cha kuanzia kampeni mpaka matokeo yanapotangazwa na nchi inakuwa salama; tunaangalia utayari wa askari wetu katika rasimali watu, vitendea kazi pamoja na elimu na utayari wa jumla kwa jamii," alisema Kidavasha.
Pichani ni kiongozi huyo alipokutana na Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bi. Miriam Mmbaga akiwa ameambatana na viongozi wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Simiyu akiwepo Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Simiyu, Henry Mwaibambe.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-http://simiyuregion.blogspot.com/2020/08/blog-post_27.htm
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa