Mkuu wa wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, Mhe. Aswege Kaminyoge amezindua bodi ya Kampuni ya Ng'hami (Ng'hami Industries Company Ltd), ambayo iko chini ya Halmashauri ya wilaya ya Maswa itakayoendesha viwanda vinavyomilikiwa na halmashauri hiyo.
Akizindua bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo jana katika ukumbi wa Halmashauri ya Maswa mkuu huyo wa wilaya amesema uzinduzi wa bodi hiyo unaashiria utekelezaji wa dhamira njema ya kuwa na viwanda vya kimkakati ndani na nje ya Mkoa wa Simiyu.
Kaminyoge amesema matokeo ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati kwa sekta ya viwanda Wilayani Maswa yameanza kuonekana dhahiri kwa vitendo na kukuza uchumi wa wananchi wao kwa ujumla.
Bodi hiyo itasimamia viwanda vitano ambavyo ni kiwanda cha kusindika Unga lishe wa viazi,Kiwanda cha Chaki,Kiwanda cha vifungashio ,kiwanda cha unga wa gypsum na cha kutenga madaraja ya mchele.
MWISHO
KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/08/dc-maswa-azindua-kampuni-itakayosimamia.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa