• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

DC Bariadi Aaagiza Mkandarasi Aliyetelekeza Mradi Akamatwe

Posted on: February 15th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kumtafuta  mkandarasi wa Kampuni ya LNGA na kumpeleka Polisi ili akatoe maelezo ya sababu za kutelekeza kazi ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 28 na kukiuka masharti ya mkataba.

Kiswaga alitoa agizo hilo wakati wa zoezi la kutia saini mikataba 16 ya ujenzi wa barabara na madaraja kati ya Wakandarasi na Mameneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA)  wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu., ambapo alishuhudia zoezi hilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka.

Kiswaga amesema amekuwa akimtafuta mkandarasi huyo ili wakae pamoja kujua sababu za kutelekeza na kuchelewesha ukamilishaji wa mradi huo lakini amekuwa  akikaidi wito na maagizo ya Serikali , hivyo ipo haja afikishwe katika jeshi hilo ili aweze kutoa maelezo.

“Mhandisi alinieleza mwenendo wa kazi yake nikamwita Ofisini tukamwonya, nilienda kutembelea mradi sikumkuta nikampigia simu hapokei, hii wiki ya tatu hapokei simu yangu wala ya Mhandisi, naagiza huyu mkandarasi LNGA atafutwe apelekwe polisi ili atueleze anatekeleza mradi wa Serikali au barabara ya nyumbani kwake” alisema Kiswaga.

Meneja wa TARURA wa Halmashauri ya Bariadi Vijijini Mhandisi. Masatu Ndango amesema amepokea maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ya kumtafuta mkandarasi LNGA, anayefanya kazi ya matengenezo ya barabara ya Mbiti-Sakwe-Itubukilo (KM 17), Sakwe-Mbiti(KM 4), Sakwe-Pugu (KM 3) na Ngulyati-Mwanzoya (KM 4) ambaye kwa mujibu wa mkataba alipaswa kukamilisha kazi Desemba 2017.

Ndango amesema Mkandarasi huyo amekuwa akikaidi maelekezo kila anapoelezwa na ameshindwa  kukamilisha mradi kwa wakati,  hivyo kwa mujibu wa mkataba ameanza kukatwa Fedha ambazo ni adhabu ya ucheleweshwaji wa mradi(Liquidated damage).

Kutokana na hali hiyo Mkuu wa Wilaya, Mhe.Festo Kiswaga amesema Wakandarasi wa aina hiyo hawana na nafasi katika Mkoa wa Simiyu na kamwe wasifikirie kuwa mkoa huo ni mahali pa kujifunzia, hivyo akawataka Wakandarasi wote 16 waliosaini mikataba ya ujenzi wa barabara na madaraja kupitia TARURA kuheshimu kazi wanazopewa na Serikali.

Aidha, amewataka Mameneja wa TARURA mkoani Simiyu kuhakikisha wanajiridhisha na uwezo wa wakandarasi wote watakaotekeleza miradi mkoani humo, ili miradi yote itekelezwe kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Akiwasilisha taarifa kwa niaba ya Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Meneja wa TARURA Halmashauri ya Mji Bariadi Mhandisi.Mathias Mugolozi amesema jumla ya mikataba itakayotekelezwa ni 16 ikiwa na thamani ya shilingi 1, 830, 524,724.91, ambapo Halmashauri ya Mji ina mikataba miwili(02), Bariadi Vijijini miwili(02), Itilima miwili(02), Busega miwili(02), Meatu miwili(02) na Maswa mikataba sita(06).

Kwa upande wake Mratibu wa TARURA Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Peter Mosha amesema TARURA mkoa  pamoja na Mameneja wa TARURA wa Halmashauri wamejipanga na watahakikisha wanatembelea miradi yote mara kwa mara na kufanya vikao vya ndani kwa lengo la kufanya tathmini ya maendeleo ya miradi hiyo.

Naye Mkandarasi Fahmy Hemed kutoka Kampuni ya Hemed Holdings Ltd ya Mkoani Shinyanga amesema watahakikisha wanafanya kazi katika viwango vya ubora vinavyohitajika, kukamilisha kwa wakati  na kuheshimu mikataba.

Miradi hii 16 ni ya kwanza kutekelezwa Mkoani Simiyu chini ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),  tangu kuanzishwa kwa Wakala huo kupitia Tangazo la Serikali la tarehe 12/05/2017 na kuzinduliwa rasmi tarehe 02/07/2017.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/02/serikali-mkoani-simiyu-yaagiza.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa