• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Darasa la Saba Simiyu Waomba Wasimamizi Wenye Tabia ya Kuwatisha Watahiniwa Waache

Posted on: August 27th, 2018

Wanafunzi wa darasa la saba shule za msingi za Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wamemuomba Mkuu wa Mkoa, Mhe Anthony Mtaka, kuwataka  wasimamizi wa Mtihani wa Taifa wenye tabia ya kuwatisha wanafunzi wakiwa katika chumba cha mtihani waache tabia hiyo ili wanafunzi wafanye Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba, mwaka 2018 kwa uhuru pasipo uoga.

Wanafunzi hao wametoa ombi hilo Agosti 27, 2018, wakati Mkuu Mkuu huyo wa Mkoa alipokutana na wanafunzi wa darasa la saba takribani 782 wa shule tano za msingi za Mjini BARIADI, katika Shule ya Msingi Sima B, lengo likiwa ni kuwahimiza kusoma kwa bidii katika siku chache zilizobakia na kuwatakiwa kila la heri katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Septemba 05 na 06, 2018.

Wamesema kuwa wamepata taarifa kutoka kwa wenzao waliowatangulia kuwa siku za nyuma kulikuwa na baadhi ya wasimamizi wa Mtihani wa Darasa la Saba ambao walikuwa wakiwatisha na kuwanyanyasa watahiniwa, hivyo kuwafanya wanafunzi kufanya mtihani wakiwa na hofu jambo lililofanya baadhi yao kushindwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao.

“ Miaka ya nyuma tunasikia kuna wasimamizi walikuwa wanawatishia sana wanafunzi, tunaomba  Mkuu wa mkoa utusaidie na sisi wasije wakatutishia tukashindwa kufanya mtihani wetu wa Taifa vizuri” alisema John Isack Mwanafunzi wa darasa la Saba Shule ya Msingi Sima A, Bariadi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewahakikishia wanafunzi hao kuwa hakutakuwa na vitisho wala manyanyaso yoyote kutoka kwa wasimamizi wa mitihani na akawaeleza kuwa atakutana na wasimamizi wa mitihani ambao wapo katika semina elekezi na kuwapa angalizo hilo.

“Nikitoka hapa sasa hivi naenda kuongea na wasimamizi wa mitihani, niwahakikishie tu kwamba hamtatishwa msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni kujisomea mjiandae vizuri na mtihani na mkiwa kwenye chumba cha mtihani mkawe watulivu na kumwomba Mungu awakumbushe yote mliyokuwa mnajisomea” alisema Mtaka.

Akizungumza na wasimamizi wa Mtihani wa Darasa la Saba, Mtaka amewataka wasimamizi hao ambao ni walimu kuwasimamia wanafunzi hao huku wakitambua kuwa wao ni walezi, hivyo wanapaswa kusimamia kwa kufuata taratibu zilizowekwa pasipo kuwatisha wala kuwanyanyasa watahiniwa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni moja kwa mwanafunzi wa kiume, milioni moja na laki tano kwa mwanafunzi wa kike atakayekuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa katika Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba mwaka 2018 na shilingi milioni tatu kwa Shule ya Msingi ya Mkoa huo itakayokuwa miongoni mwa shule kumi bora Kitaifa.

Nao wanafunzi wa Darasa la Saba Mjini Bariadi wamemhakikishia mkuu wa mkoa kuwa watafanya vizuri katika Mtihani wa Taifa kwa kuwa wameandaliwa vizuri na walimu wao katika shule zao na katika kambi za Kitaaluma walizokaa kwa siku 21 mwezi Juni kujiandaa na mtihani huo.

“Tunakushukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa kutuwezesha kuwa na kambi za kitaaluma, zimetusaidia kutuandaa na mtihani wa Taifa maana tulijifunza vitu vingi, tukapata maarifa mapya, sasa pia hivi walimu wetu wametuandaa vizuri tuko tayari kwa Mtihani wa Taifa, tunakuahidi tutafanya vizuri” alisema Hilda Mgalula Mwanafunzi wa darasa la saba Sima B.

Afisa Taaluma Mkoa wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime amesema jumla ya watahiniwa elfu 35 Mkoani Simiyu wanatarajia kufanya mtihani wa darasa la saba Septemba tano na sita, mwaka 2018.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/08/darasa-la-saba-simiyu-waomba-wasimamizi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa