• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Darasa la Saba Simiyu Waahidi Kuongoza Mtihani wa Taifa Mwaka 2020

Posted on: October 5th, 2020

Zikiwa zimebaki siku mbili wanafunzi wa darasa la saba nchini  kufanya mtihani wa Taifa, wanafunzi wa darasa la saba mkoani Simiyu wamesema wamedhamiria kushika nafasi ya kwanza Kitaifa  katika mtihani huo kutokana na mikakati ya taaluma iliyopo na maandalizi yaliyofanyika, huku wakiahidi pia kutoa wanafunzi kumi bora Kitaifa.

Hayo yamebainishwa Oktoba 05, 2020 na baadhi ya wanafunzi wa Shule za msingi Somanda A, Somanda B, Sima A na Sima B za mjini Bariadi wakati wa ziara ya Viongozi wa Mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika shule hizo iliyokuwa na lengo la kujiridhisha na maandalizi na kuwatakia heri wanafunzi watakaofanya mtihani huo.

“Tumejiandaa vizuri na mtihani wa Taifa utakaofanyika tarehe 07 na 08 mwezi huu, walimu wetu wametuandaa vizuri tunawashukuru sana walimu kwa kutufundisha vizuri, tulifanya vizuri mtihani wa Mock na tumejipanga kufanya vizuri zaidi mtihani wa Taifa, tunaahidi kutoa wanafunzi watano katika  kumi bora Kitaifa,” Kija Masunga mwanafunzi wa darasa la Saba Somanda B.

“Nawashukuru walimu kwa kutufundisha kutoka chekechea mpaka darasa la saba pia tunashukuru uwepo wa kambi za kitaaluma zimetusaidia sana, baadhi ya wanafunzi katika shule za serikali wanadanganywa na wazazi wao wakaandike majibu yasiyo sahihi ili wakaozeshwe lakini kupitia kambi wanafunzi tunalindwa na tunajiamini,”Edina Meshaki kutoka Sima A.

Aidha, wanafunzi hao wameomba Serikali iendelee kuboresha miundombinu ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na uwekaji wa nishati ya umeme katika vyumba vyote vya madarasa ili waweze kujisomea nyakati zote hususani wakati wa kambi za kitaaluma.

Mwalimu Monica Silayo kutoka Shule ya Msingi Somanda B amesema wamewaandaa wanafunzi vizuri ambapo amebainisha kuwa wanafunzi hao wako tayari  kufanya mtihani huo wa Taifa bila wasiwasi wowote.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sima A, Hamza Hamis amesema “sisi si watu wa maneno ni watu wa vitendo hatuzungumzi mambo mengi lakini tunaahidi kuwa tumejipanga; hili suala la kuwa namba moja tumeliwekea mikakati toka mwaka jana  sasa hivi tunafanya mwendelezo wa mikakati yetu na mwaka huu Simiyu hatukamatiki”.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewashukuru walimu wote wa mkoa wa  Simiyu kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka viongozi na watumishi wengine kutoa kipaumbele kwa walimu katika maeneo ya huduma ili wapata nafasi ya kuwafundisha wanafunzi wao .

Kuhusu zawadi kwa wanafunzi na walimu watakaofanya vizuri katika mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba mwaka 2020 Mtaka amesema, “wanafunzi watakaoingia 10 Bora kitaifa kila mmoja atapewa shilingi 500,000/= mwalimu atakayeongoza kwa ufaulu wa A nyingi kimkoa katika kila somo atapewa shilingi 500,000/=, shule itakayoingia 10 bora Kitaifa itapewa shilingi milioni tatu, wilaya itakayoingia 10 bora walimu wake wataenda kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.”

Mtaka ameongeza kuwa katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la saba mwaka 2019 wanafunzi mkoa wa Simiyu ulitoa wanafunzi wanne walioingia katika 10 bora Kitaifa kwa shule za Serikali na kila mwanafunzi aliepwa zawadi ya shilingi 300,000/=

Kwa mujibu wa Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju jumla ya wanafunzi 30,779 wanatarajia kufanya mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba, huku akibainisha kuwa maandalizi yako vizuri ambayo yamechangiwa na walimu, wazazi, viongozi na wadau wote wa elimu kwa lengo la kufikia azma ya mkoa ya kushika nambari moja Kitaifa.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI TEMBELEA BLOGU YETU TA MKOA KWA KIUNGANISHI HIKI:- https://simiyuregion.blogspot.com/2020/10/darasa-la-saba-simiyu-waahidi-kuongoza.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa