• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

CWT Kujenga Kiwanda cha Mikate Lishe Simiyu

Posted on: November 29th, 2019

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kinatarajia kujenga kiwanda cha mikate lishe kupitia kampuni yao inayosimamia Maendeleo ya Walimu ya biashara (TDCL), katika eneo la Ng’hami wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Akimkabidhi  Katibu wa Chama cha Walimu Nchini, Mwl. Deus Seif hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2), Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe amesema wilaya imetoa kiwanja hicho bure, ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda ambapo kumhakikishia upatikanaji wa malighafi ya kiwanda hicho (viazi lishe)

“Tumejipanga kuzalisha viazi lishe vya kutosha vitavyotumika kama malighafi ya kiwanda hiki na tayari wakulima wamepewa mbegu za viazi hivyo, niendelee kuwakaribisha CWT wilayani Maswa, kama kuna uwekezaji mwingine mnahitaji kufanya karibuni, hata kama ni tawi la benki yenu ile ya walimu tunawakaribisha sana,” alisema Dkt. Shekalaghe.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Simiyu amesema kukamilika kwa kiwanda hicho kutasaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa lishe ambalo limekuwa ni changamoto kwa  Mkoa wa Simiyu.

Aidha, Mtaka amesisitiza Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashautri na wataalam wa kilimo wahakikishe mbegu ya viazi lishe inapatikana kwa wingi ili wananchi wanapohitaji waipate

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Taifa, Mwl. Deus Seif amesema chama hicho kinaunga mkono sera ya Tanzania ya Viwanda huku akibainisha kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utaenda haraka kwa kuwa tayari kampuni ya CWT inayosimamia miradi imeshaanza kulifanyia kazi suala hilo.

Ameongeza kuwa pamoja na kujenga kiwanda cha mikate lishe, chama hicho pia kinatarajia kuchukua uwakala katika Kiwanda cha Chaki cha Maswa ili kusambaza chaki zinazozalishwa wilayani humo katika shule zote nchini.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/11/cwt-kujenga-kiwanda-cha-mikate-lishe.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa