• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

CUAMM Yajenga Jengo la Huduma kwa Watu Wenye VVU Simiyu

Posted on: June 19th, 2020

Shirika lisilo la kiserikali la Doctors With Africa - CUAMM kupitia Mradi wa Test and Treat limejenga jengo jipya la huduma za tiba na matunzo kwa watu wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, kukarabati baadhi ya majengo na kuchimba kisima cha maji  katika zahanati ya Old Maswa iliyopo Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo (katika zahanati ya Old Maswa  inayomilikiwa na  Jimbo Katoliki Shinyanga)   Juni 18, 2020  kwa niaba ya Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Liberatus Sangu,  Makamu wa Askofu huyo Padri Kizito Nyanga,  ameishukuru Doctors with Africa- CUAMM kwa msaada huo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau wote walio tayari kuhudumia watu.

“Tunawashukuru sana CUAMM kwa msaada wa jengo hili, vifaa na ukarabati wa majengo mengine katika zahanati ya Old Maswa; Kanisa lina kiu ya kuwafikia watu kwa huduma siyo maneno na liko tayari kushirikiana na wote wanaotaka kuwahudumia watu,” alisema Padri Nyanga.

Aidha, Padri Kizito ameishukuru serikali kwa kuliamini kanisa hususani jimbo Katoliki Shinyanga, kuliamini kanisa katika kutoa huduma kwa wananchi, kulidhamni katika kuendeleza huduma na kutoa ushauri wa mara kwa mara katika uendeshaji wa taasisi za kanisa.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali katika uzinduzi wa jengo hilo Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt.Khamis Kulemba amesema CUAMM ni miongoni mwa wadau ambao wanafanya kazi kulingana na malengo ya serikali ya mkoa ya kuboresha miundombinu katika sekta ya afya.

Wakati huo huo Kulemba amewataka wataalam afya katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa kushirikiana na watumishi wa Zahanati ya Old Maswa kuhakikisha huduma zinazotolewa katika jengo hilo la CTC na zahanati hiyo kwa ujumla zinakuwa ni za ubora unaotakiwa  na ziendane na thamani ya mradi huo.

Katika hatua nyingine Dkt. Kulemba ametoa wito kwa viongozi wa Dini mkoani Simiyu kuendelea kushirikiana na wataalam wa afya katika kulinda afya ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi(VVU),  wanaotumia dawa za kufubaza makali ya VVU katika kuwahimiza watumie dawa hizo kwa usahihi badala ya kuwataka kuacha kutumia dawa hizo baada ya kuwaombea.

“Nawaomba viongozi wa dini washirikiane na wataalam kulinda afya za watu wenye VVU, baadhi yao wamekuwa wakiwaombea watu wenye VVU na kuwaambia waache kutumia dawa; watu hao wakiacha kutumia dawa wanakuwa na hali mbaya; kuacha kutumia dawa na kuzirudia tena kunawaletea shida na kutengeneza usugu, nawaomba viongozi wa dini watusaidie kwenye hili,” alisema Kulemba.

Naye Mganga mfawidhi wa zahanati ya Old Maswa Ndaro Lawi amesema huduma za tiba na matunzo kwa watu wenye Virusi vya Ukimwi (VVU) katika zahanati hiyo zilianza mwaka 2016, ambapo hadi sasa  jumla ya watu 219 wameandikishwa katika kituo hicho na  wanapata huduma mbalimbali bila malipo.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa Test and Treat kutoka Doctors With Africa- CUAMM  mikoa ya Shinyanga na Simiyu, Ndg. Ndg. Franscesco Bonanome amewashukuru viongozi wa Serikali, Jimbo Katoliki Shinyanga na watumishi wa CUAMM, kwa namna walivyofanya kazi kwa ushirikiano na kuahidi kuwa shirika hilo litaendelea kufanya mambo makubwa siku za zijazo.

Ujenzi wa Jengo la CTC na ukarabati wa majengo mengine katika Zahanati ya Old Maswa umegharimu shilingi 209, 885, 665/= huku uchimbaji wa kisima ukigharimu shilingi 39,533,540/=

MWISHO

KWA PICHA ZAIDI FUNGUA LINKI HII:-http://simiyuregion.blogspot.com/2020/06/cuamm-yajenga-jengo-la-huduma-kwa-watu.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa