• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Chuo cha Mipango Washukuru Uongozi Mkoa wa Simiyu kuwapatia Eneo la kujenga Tawi jipya Bariadi

Posted on: May 26th, 2018

Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango Dodoma limeushukuru , uongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa kukubali kutoa eneo la ekari 50 bure kwa ajili ya ujenzi wa Tawi jipya la chuo hicho , katika Kata ya Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Shukrani hizo zimetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango Bibi.Mugabe Mtani , katika mazungumzo maalum na viongozi wa Mkoa wa Simiyu muda mfupi kabla ya kikao cha Baraza hilo kilichofanyika mkoani Simiyu.

Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango Bibi. Mugabe Mtani ameshukuru kwa niaba ya Chuo hicho  kwa kupewa eneo hilo ambalo litawawezesha kujenga miundombinu ya kutosha ya chuo hicho katika Mkoa wa Simiyu.

 “Tunashukuru sana uongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa kutupa hili eneo kubwa katika wakati huu ambao sisi tunaona ni wakati muafaka kwa sababu tulikuwa kwenye mkakati wa kutafuta eneo la kujenga, pale Mwanza tuna eneo ambalo kama tungelitumia lingetugharimu fedha nyingi kuliko hili la Simiyu kwa sababu liko kwenye mawe” alisema Mtani.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango, Hozen Mayaya amesema iwapo chuo hicho kitakamilika kujengwa kitasaidia kutoa mafunzo ya maendeleo vijijini na hivyo kusaidia upatikanaji wa watalaam hapa nchini wakiwemo wa mipango pamoja na kusaidia katika ufanyaji wa tafiti mbalimbali.

Ameongeza kuwa upatikanaji wa eneo hilo utasaidia lengo la Chuo la kuwa vituo vingi kadri mahitaji yanavyoongezeka jambo ambalo litasaidia pia kusogeza huduma karibu na wananchi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambako eneo hilo lipo, Bw. Melkizedeck Humbe amesema Chuo cha Mipango kitapojengwa Mkoani Simiyu kitakuwa msaada mkubwa kwa Mkoa huo ambao unajipambanua kwa Uchumi wa viwanda.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwepo kwa chuo hicho kutaongeza hamasa ya elimu kwa vijana wanaomaliza elimu ya sekondari na kidato cha sita kujiunga na vyuo vya elimu ya juu ,huku akitoa wito kwa Taasisi zingine za umma na binafsi kuwekeza katika sekta ya elimu.

“ Sisi kama Mkoa tunatoa fursa kwa Wakuu wote wa Vyuo Vikuu hapa nchini wanaotaka kujenga matawi ya Vyuo vyao ili waondokane na kulipa fedha nyingi kwa ajili ya pango la majengo, mkoa wa Simiyu unawaakaribisha na tunawahakikishia upatikanaji wa Ardhi Bure” alisema Mtaka.

MWISHO:

 

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/05/chuo-cha-mipango-washukuru-uongozi-mkoa.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa