Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani, Mfuko wa Mabadiliko tabia nchi (CGF) na wananchi, imetenga kiasi cha shilingi bilioni 375.4 kutekeleza Mradi wa kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi mkoani SIMIYU kwa awamu ya kwanza, ambao utakuwa suluhisho la kudumu la tatizo la maji mkoani humo
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe wakati akifungua kikao cha wadau wa mabadiliko ya tabia nchi kilichofanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri Kamwelwe amesema moja ya shughuli muhimu na kubwa katika utekelezaji wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi, ni ufikishaji wa huduma ya Maji ya Ziwa Victoria katika Mji wa Bariadi , Busega na Itilima kwa awamu ya kwanza na baadaye katika Wilaya ya Meatu na Maswa.
Ameongeza kuwa upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Simiyu uko chini ikilinganishwa na wastani wa Kitaifa na kwa kutambua hali hii, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ilibuni mradi huu, ili kupata suluhisho la kudumu la tatizo la maji kwa wananchi na mifugo ambayo ni moja ya shughuli za kiuchumi za wananchi wa Mkoa wa Simiyu.
Aidha, Waziri Kamwelwe amesema lengo la mradi huu ni kuboresha Afya na kuongeza uzalishaji maji ili kuinua hali ya maisha kwa wananchi walioathirika na mabadiliko ya tabia nchi, ambapo amebainisha kuwa katika kufikia lengo shughuli mbalimbali zitatekelezwa katika nyanja za maji safi na usafi wa mazingira, kilimo endelevu na ufugaji.
Waziri pia amebainisha kuwa kutakuwa na ujenzi wa mabwawa ya kilimo cha umwagiliaji endelevu na maji ya mifugo, ujenzi wa mabwawa ya kutibu maji taka pamoja na vyoo vya mfano katika Shule na Vituo vya Afya.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo ambao utawasaidia wananchi wa mkoa huo na utakuwa chachu katika Ujenzi wa Viwanda mkoani humo kwa kuwezesha upatikanaji wa maji ya uhakika.
“Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wote wanausubiri sana mradi huu wa maji ya Ziwa Victoria; pia Mkoa wetu unaenda kwenye uwekezaji wa viwanda vikubwa na changamoto tuliyonayo ni suala la upatikanaji wa maji ya uhakika, utekelezaji wa mradi huu utatusaidia sana katika viwanda” amesema Mtaka.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa Simiyu ni Miongoni mwa Mikoa yenye kiwango cha chini cha upatikanaji wa huduma ya maji ambayo Serikali imetoa kiupaumbele cha kuipa fedha kutoka katika Fedha za Mfuko wa Maji ili kutekeleza miradi ya maji itakayoibuliwa na kuwasilisha maandiko yake wizarani.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amewahimiza Wataalam wa Halmashauri kwa kushirikiana na Mkoa kuandaa maandiko ya kuibua miradi ya Maji itakayowasilishwa wizara ya maji, kwa lengo la kuomba fedha za kutekeleza miradi hiyo ili kuongeza na kuboresha upatikanaji wa huduma za maji mkoani humo.
Mradi wa kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi Mkoani SIMIYU ambao zabuni yake imepangwa kutangazwa Januari 2018; utatekelezwa kwa awamu mbili awamu ya kwanza utaanza na Mji wa Bariadi, Busega na Itilima pamoja na vijiji 278 vilivyopo pembezoni mwa bomba kuu umbali wa Kilomita 12 kila upande, baadaye maeneo mengine ya Wilaya za Maswa na Meatu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi (hawapo pichani) unaotekelezwa Mkoani humo, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na Wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi (hawapo pichani) unaotekelezwa Mkoani Simiyu kwenye kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi, unaotekelezwa Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
Baadhi ya wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi unaotekelezwa Mkoani Simiyu akifuatilia masuala mbalimbali yalikuwa yakijadiliwa katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
Baadhi ya wadau wa Mradi wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Mabadiliko ya Tabianchi unaotekelezwa Mkoani Simiyu akifuatilia masuala mbalimbali yalikuwa yakijadiliwa katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo.
KWA PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILI BOFYA HAPA CHINI
https://simiyuregion.blogspot.com/2017/11/bilioni-3754-zatolewa-kutekeleza-mradi.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa