• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Benki Ziwasaidie Wakulima Kupata Elimu kwa Kuwafuata Walipo: RC Malima

Posted on: August 8th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima ametoa wito kwa taasisi za fedha zikiwemo benki kuwafuata wakulima na kuwapa mafunzo yatakayowasaidia ikiwemo mafunzo ya utunzaji, usimamizi wa fedha na namna ya kupata mikopo ya kuwasaidia katika kuongeza tija ya kilimo.

Mhe. Malima ameyasema hayo Agosti 07, 2020 wakati alipotembelea mabanda mbalimbali katika maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2020 ambayo yamefanyika katika uwanja wa Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.

“ Elimu ambayo benki inatoa kwa wakulima na AMCOS ni nzuri sana kwani imesaidia sana nchi za Mashariki ya mbali ‘Far East’ wapate mafanikio makubwa sana; nafarijika sana na NMB Foundation kwa kuwafuata wakulima huko huko waliko vijijini,” alisema Malima.

Kwa upande wake Meneja wa NMB kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Sospeter Magesse amesema madarasa ya wakulima yalianza toka 2019 kukiwa na Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) 30, mwaka huu benki hiyo imefanikiwa kuendesha mafunzo kwa AMCOS 50.

Aidha, Magesse ameongeza kuwa benki ya NMB kupitia NMB Foundation imekuwa ikiwafikia wakulima mahali walipo  vijijini na kuwafanyia mafunzo ambapo mwaka 2019/2012 jumla ya AMCOS 1520 zimepatiwa mafunzo na NMB foundation.

Akizungumza na watumishi wa wizara ya fedha na mipango mara baada ya kutembelea banda la wizara hiyo Mhe. Malima ameipongeza wzara hiyo kwa namna ilivyoboresha hali ya usimamizi wa mali za umma na nidhamu ya matumizi ya fedha za Umma huku akitoa wito kwa wizara kuona aina za kodi zinazoweza kumnufaisha mkulima na kuachana na kozi ambazo hazina manufaa kwa mkulima.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima, mgunduzi wa viuadudu viitwavyo VURUGA Dkt. Never kutoka Chuo cha Nelson Mandela amesema

amefanikiwa kutengeneza viuadudu hivyo ambayo vinasaidia sana kuzuia mazao kushaambuliwa na wadudu waharibifu hususani kwenye pamba.

Mhe. Malima pamoja na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Bi. Mary Makondo walipata fursa ya kutembelea mabanda ya wizara, taasisi, mashirika mbalimbali pamoja na mabanda ya wajasiriamali kujionea bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wajasiriamali hao na kujionea jinsi Wakulima, Wafugaji, Wavuvi na taasisi mbalimbali zinavyofanya kazi ili kuhakikisha tunafikia Tanzania ya Viwanda Kupitia Kilimo.

Maonesho ya Nanenane mwaka 2020 yanabebwa na Kauli Mbiu isemayo, “KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020.”

MWISHO.

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:https://simiyuregion.blogspot.com/2020/08/benki-ziwasaidie-wakulima-kupata-elimu.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa