• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Balozi wa Indonesia, Waziri Kigwangalla Watembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa Mkoani Simiyu

Posted on: August 4th, 2019

Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mhe.  Prof. Dkt..Ratlan Pardede na  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla Agosti 04, 2019 wametembelea Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu.

Akizungumza mara baada ya kuwapokea wageni hao Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema asilimia 80 ya uchumi wa nchi unategemea kilimo, hivyo kwa kuwa Mhe.Kigwangalla ni Waziri mwenye Dira kwa kutembelea maonesho haya atatoa mchango,mawazo na hamasa kubwa kuhusiana na sekta ya kilimo.

Aidha, amesema Prof.Dkt.Ratlan Pardede amekuja kwa mara ya pili sasa Mkoani Simiyu, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Indonesia na Mkoa wa Simiyu (Tanzania.)

Naye Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Dkt.Hamisi Kigwangalla amepongeza waandaji wa maonesho haya ya Nanenane Kitaifa (Kanda ya Ziwa Mashariki) kwa maandalizi mazuri ya pia amewapongeza Wakulima na Wafanyabiashara kwani kwa kushiriki maonesho haya wanapata fursa ya kujifunza na kuuza mazao yao.

Amesema sekta ya kilimo ni sekta muhimu kwani ndiyo sekta inayoajiri wananchi wengi ikifuatiwa na sekta ya utalii na inategemewa na Uchumi wa Viwanda kutoa malighafi za viwanda, huku akibainisha kuwa Utalii unachangia pato la Taifa kwa asilimia 17.6 , pia unachangia kwa zaidi ya 25% ya upatikanaji wa fedha za kigeni.

.

Mhe. Kigwangalla ameongeza kuwa mwaka 2015 kulikuwa na ongezeko la Watalii kutoka Milioni 1 hadi milioni 1.1, .Mwaka 2018 Watalii waliongezeka hadi kufikia Milioni 1.6 na lengo likawa ni kufikia mwaka 2020 idadi iongezeke zaidi na kufikia watalii milioni mbili.

Naye Balozi wa Indonesia Prof.Dr.Ratlan Pardede amesema amefurahi kufika Mkoani Simiyu kwa mara ya pili sasa na Indonesia inashiriki Maonesho ya Nanenane ili kuimarisha uhusiano wake na Tanzania hususani katika kilimo.

“Nimefura sana kufika kwa mara ya pili sasa mkoani Simiyu tunashiriki  Nanenane kwa sababu tunataka kuimarisha uhusiano wetu na Mkoa wa Simiyu hususani katika kilimo, kusudi likiwa ni kuona kwa jinsi gani tunaweza kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa katika siku za usoni kwa manufaa ya nchi zote mbili yaani Tanzania na Indonesia” alisisitiza.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/08/balozi-wa-indonesi-waziri-kigwangalla.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa