• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Balozi wa Indonesia Aahidi Kuwaalika Wawekezaji wa Viwanda vya Nguo, Ngozi na Mbolea Kuwekeza Simiyu

Posted on: May 15th, 2018

Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof.Dkt. Ratlan Pardede amewaahidi viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuwa atawaalika wawekezaji wa Viwanda vya nguo, viwanda vya kuchakata ngozi  na viwanda vya kutengeneza  mbolea kutoka nchini Indonesia kuja kuwekeza Mkoani Simiyu.

Mhe. Balozi Pardede ameyasema hayo Mei 15, alipokuwa katika ziara yake Mkoani Simiyu mara baada ya kutembelea kiwanda cha Kuchambua pamba cha Kasoli Alliance kilichopo Wilayani Bariadi na Kiwanda cha kuchakata ngozi cha Senani wilayani Maswa.

Amesema atawaalika wafanyabiashara kutoka nchini Indonesia kuja Simiyu ili wakutane na viongozi wa mkoa huo pamoja na wafanyabiashara wenzao kujadili juu ya kuongeza uzalishaji wa pamba bora, bei ya pamba na kuona namna ya kuuza pamba ya Simiyu (Tanzania) nchini Indonesia moja kwa moja.

Pamoja na kuahidi kuwaalika wawekezaji wa viwanda vya kuchakata bidhaa za ngozi, Balozi Pardede akiwa katika kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Senani Maswa ameahidi kusaidia kuleta wataalam kutoka Indonesia watakaosaidia wafanyakazi wa kiwanda kutengeneza bidhaa bora za ngozi na kuwapeleka wafanyakazi hao Indonesia kujifunza na kupata maarifa na uzoefu.

Meneja mkuu wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Bw. Boaz Ogola amesema ujio wa Balozi wa Indonesia ni fursa kubwa kwa wanunuzi wa pamba kutokana na nchi hiyo kuwa na uhitaji mkubwa wa pamba kwa ajili ya viwanda vya nguo na utafungua milango ya majadiliano na wafanyanyabiashara wa Indonesia na kufanya biashara ya moja kwa moja.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema wamezungumza na Mhe.Balozi kumuomba awaalike wafanyabiashara wa Indonesia Mkoani humo kuwekeza kwenye viwanda vya kuchakata ngozi, ili viwanda vidogo vilivyopo na vitakapojengwa viwanda vikubwa uwekezaji wake uanze na malighafi kutoka ndani ya mkoa.

Aidha, Mtaka amesema Simiyu kama mkoa unaojihusisha na kilimo na unaopakana na mikoa inayofanya shughuli za kilimo unaona ipo haja ya kuwa na wawekezaji wanaotengeneza mbolea jambo ambalo limepokelewa na Mhe. Balozi na kuahidi kulifanyika kazi kwa kuwaalika wawekezaji.

“Tumezungumza na Mhe. Balozi na ameona uhitaji na umuhimu wa kuwakaribisha wawekezaji kulingana na mkoa jinsi ulivyo, jambo hili la kupata wawekezaji kwenye uzalishaji wa mbolea lipo pia katika mwongozo wetu wa uwekezaji kwa ajili ya kusaidia mikoa inayotuzunguka kama sehemu ya kuboresha eneo la kilimo” alisema.

Wakati huo huo Mtaka amesema wamezungumza na Mhe. Balozi kuona uwezekano wa kutoa nafasi kwa Mkoa wa Simiyu kuwa mwenyeji wa mkutano kati ya Wizara ya Kilimo ya Indonesia na Wizara ya kilimo ya Tanzania ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Mhe.Balozi alipata nafasiya kutembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa, ambapo Mkuu wa Mkoa amesema Serikali imetoa shilingi bilioni 8.2 kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda hicho na ujenzi wa kiwanda cha vifungashio, hivyo akawataka vijana wanaofanya kazi katika kiwanda hicho kufanya kazi kwa bidii ambapo amewahakikishia kuwa baada ya upanuzi wa kiwanda hicho watakuwa waajiriwa wa kudumu.

Mhe. Balozi bado anaendelea na ziara yake mkoani Simiyu ambapo amepatata nafasi ya kutembelea kiwanda cha kuchambua pamba Kasoli Alliance, Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi na kiwanda cha chaki wilayani Maswa.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUGUA KIUNGANISHI HIKI HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/05/baloziwa-indonesia-hapa-nchini-prof.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa