• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

ATAPE Kuwekeza kwenye Miradi ya Maji, Ujenzi wa Hosteli Simiyu

Posted on: April 17th, 2019

Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE), kinakusudia kuwekeza katika ujenzi wa mradi wa maji kuunga mkono juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi  na ujenzi wa hosteli ili kutoa huduma za malazi katika Mkoa wa Simiyu.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Freddie Manento,  Aprili 17, 2019 wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi, ambako unafanyika Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama hicho kwa takribani siku saba ambao umeanza Aprili 16 na utahitimishwa Aprili 21, 2019.

Manento amesema  ATAPE imedhamiria kuwekeza kwenye miradi itakayokuwa na tija kwa Watanzania wote kwa ujumla huku akieleza kuwa timu ya wataalam wa uwekezaji wa chama hicho inaendelea kufanya utafiti, ili kubaini eneo litakalofaa kuchimba kisima cha maji na kujenga hosteli mkoani Simiyu.

“Tumedhamiria kuacha alama katika Mkoa wa Simiyu kupitia mkutano wetu wa 20 wa ATAPE, tumepewa fursa ya kiwanja kwa ajili ya kujenga hosteli katika kukabiliana na changamoto ya malazi, lakini pia wataalam wetu wanaendelea na utafiti kubaini mahali tutakapochimba kisima kwa ajili ya huduma ya maji kwa Wanasimiyu” alisema Manento

Pamoja na miradi hiyo inayotarajiwa kutekelezwa mkoani Simiyu, Manento amesema ATAPE imewekeza katika kilimo kwenye mashamba ya miti, miwa, mikorosho, miti ya maparachichi ambayo kwa ujumla yana ukubwa wa ekari 10,000 na ekari zaidi 3500 ambazo zinatarajiwa kufanyiwa uwekezaji mwingine.

Amesema  hadi sasa ni takribani shilingi bilioni 1.039 imewekezwa katika miradi hiyo ambayo pia imechangia kutoa ajira za kudumu na za msimu kwa Watanzania walio katika maeneo yenye miradi hiyo, huku akibainisha kuwa katika baadhi ya maeneo hayo ATAPE imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii husika.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa ATAPE ametoa wito kwa wananchi mkoani Simiyu hususani Bariadi kutumia mkutano huo kama fursa kiuchumi kupitia biashara ya bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo usafiri wa kuwatoa na kuwapeleka wajumbe katika eneo la mkutano

Kwa upande wao baadhi ya wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu wamesema Mkutano wa ATAPE umekuwa fursa kwao kwa kuwa utawasaidia kujiingizia kipato na kupata ujuzi mpya kupitia huduma na bidhaa zitakazouzwa kwenye mkutano huo.

“ Binafsi ninashukuru uwepo wa mkutano huu, mimi kama mjasiriamali nimepata pesa, nimepata ujuzi mpya kutoka kwa wenzetu waliotoka nje ya Simiyu, hivyo ninaendelea kuwaomba viongozi wetu waendelee kutuletea matukio kama haya ili tupate pesa zaidi” alisema Bw. John Bubinza mjasiriamali kutoka Bariadi.

Nao wajasirimali wanaoshiriki katika mkutano huo kutoka nje ya mkoa wa Simiyu wametoa wito kwa Wananchi mkoani Simiyu kufika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kusekwa Memorial kujifunza na kujionea kazi mbalimbali za ujasirimali ili waweze kupata ujuzi na maarifa mapya ya kufanya kazi za ujasiriamali kwa ufanisi na kununua bidhaa mbalimbali.

“ Binafsi nawakaribisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu kufika katika viwanja hivi waje wajionee, wakifika hapa watapata bidhaa kwa bei za jumla na rejareja, laikini pia nawasisitiza wanawake wainuke waje waone maana ujasiriamali unatuinua sana wanawake” alisema Mjasiriamali Esther Jichogo kutoka Jijini Dar es salaam.

Wanachama zaidi ya 1500 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato(ATAPE) wanaendelea na mkutano wao wa 20 mkoani Simiyu, ukiwa na Kauli mbiu “KUSONGA MBELE NA MUNGU” ambao utachukua takribani siku saba kuanzia tarehe  16/04/2019 hadi 21/04/2019.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII TAFADHALI BOFYA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/04/atape-kuwekeza-kwenye-miradi-ya-maji.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa