• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Askofu Lekundayo Aongoza Maombi Kumshukuru Mungu Kulivusha Taifa Katika Janga la Corona, Uchaguzi Mkuu

Posted on: December 5th, 2020

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo ameongoza viongozi na mamia ya waumini wa kanisa hilo katika ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi la Mtaa wa Ntuzu lililopo Bariadi mjini ambapo  Waumini wa kanisa hilo pamoja na wengine kutoka mkoa wa Mwanza na Mara wamewakilisha waumini wengine hapa nchini, ambapo ibada hiyo imehudhuriwa pia na viogozi wa Chama na Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

“Nilikuwa naangalia takwimu za hali ya janga la Corona ilivyo duniani leo asubuhi (Desemba 05, 2020) hadi sasa zinaonesha watu 66,281,000 wamepatwa na Corona, waliokufa mpaka sasa 1,525,294 ikiwa ulikuwa umechukulia kiurahisi, hizi takwimu zikuamshe kwamba Mungu ametupendelea sana Tanzania tunamshukuru sana Mungu kwa niaba ya wenzetu,” alisema Dkt. Lekundayo.

Awali akitoa mahubiri kabla ya maombi hayo pamoja na kuwasihi waumini kumshukuru Mungu kuwapitisha katika janga la Corona, Askofu Lekundayo pia ametoa wito kwa waumini kuendelea kumshukuru Mungu pia kwa namna ambavyo amelipitisha Taifa katika Uchaguzi Mkuu, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya jambo ambalo litabaki kumbukumbu yao juu ya neema ya Mungu katika masuala hayo.

Akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema Tanzania kupitishwa katika Janga la Corona haikuwa bahati bali ni neema ya Mungu, hivyo akawashukuru viongozi wa Dini kwa kuliombea Taifa kwa juhudi na Mungu akajibu.

Aidha, Kiswaga amesema Serikali inaendelea kuheshimu mchango wa kanisa na itaendelea kushirikiana nalo katika majukumu yake ya kitume na kimaendeleo, huku akitoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa na viongozi wake ili waweze kufanya kazi kwa manufaa na ustawi wa Watanzania.

“Katika neno la Mungu kuna habari ya wale wakoma kumi ambao waliponywa na Bwana Yesu lakini aliyerudi kushukuru ni mmoja tu, ninaamini maombi haya ya shukrani yaendelea kuiponya nchi yetu na majanga ambayo yanaonekana kwa macho na ambayo hayaonekani,” alisema Kiswaga.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Mhe. Samweli Kiboye  amesema kuna baadhi ya watu waliobeza Mhe Rais alivyotangaza  kumtanguliza Mungu kwa kutangaza siku tatu za kuliombea Taifa ili aliponye Taifa  na Janga la Corona lakini baada ya kuona matokeo ya maombi naamini wameona kuwa maamuzi yake yalikuwa sahihi.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/12/askofu-lekundayo-aongoza-maombi.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa