• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Askari Waaswa Kuepuka Vitendo Vinavyolitia Dosari Jeshi la Polisi

Posted on: February 17th, 2020

Askari mkoani Simiyu wameaswa kulinda hadhi ya jeshi la polisi kwa kujiepusha na vitendo viovu vinavyolitia dosari jeshi hilo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akizungumza na askari polisi wa mkoa huo Februari 17, 2020 ambapo amevitaja vitendo hivyo kuwa ni pamoja na kutoa siri za jeshi, kuomba rushwa, utapeli na kushiriki kuharibu ushahidi katika baadhi ya kesi.

“Ni jambo la aibu kwa askari kushiriki katika uhalifu,  kutoa siri za jeshi na kugeuka kuwa mtoa taarifa kwa wahalifu, ipendeni kazi yenu muepuke mambo yanayodhalilisha jeshi na mjenge tabia ya kuonyana ili mlinde heshima ya jeshi letu,” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka ametoa wito kwa askari polisi mkoani Simiyu kujiendeleza kielimu ili waweze kupata sifa za kulitumikia jeshi katika nafasi mbalimbali huku akiwaeleza umuhimu wa kujenga makazi na kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo Mkoani humo kwa lengo la kutengeneza kipato cha zaida.

Katika hatua nyingine  Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa Jeshi la Polisi kutenda haki kwa askari walio chini yao, ikiwemo kutoa nafasi ya kuwapandisha vyeo askari wanaostahili  kwa wakati uliopo ili kuwapa motisha katika kazi yao.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, SACP Henry Mwaibambe amesema kuwa katika Awamu hii ya tano hakuna kisingizio kwa askari kutofuata taratibu katika utendaji kazi wao.

“Zamani ilikuwa siyo rahisi sana kumkamata tajiri , lakini sasa hivi Watanzania wote tuko (level) hali moja hakuna cha huyu ni nani na yule ni nani; sasa hivi mtu asipofuata taratibu ni mapungufu yake binafsi ; tunafanya kazi kwa kufuata taratibu za jeshi pasipo kuingiliwa na mtu yeyote, sisi tuliokaa muda mrefu kwenye jeshi la Polisi tunajua kazi nzuri inayofanywa na Mhe. Rais,” alisema Mwaibambe.

Mwaibambe ameongeza kuwa askari kama watumishi wa umma wengine wanapaswa kujiepusha na masuala yanayoleta malalamiko kwa wananchi huku akisisitiza kuwa hawatasita kuwachukulia hatua askari watakaoshindwa kufanya kazi kwa uadilifu.

Kwa upande wao askari wamesema watafanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu huku wakiomba Serikali ya Mkoa iweze kuwasaidia upatikanaji wa viwanja kwa ajili ya kujenga makazi yao binafsi na maeneo ya kuweka uwekezaji wao.

“Mhe. Mkuu wa Mkoa umezungumza suala la Askari kujenga makazi, tunaomba Serikali ya mkoa ione namna ya kutusaidia kupata viwanja vya makazi katika maeneo yaliyopimwa na Halmashauri kwa gharama nafuu ili tuweze kujenga maana tunatamani kujenga Simiyu,” alisema Koplo Abdallah Manzi.

MWISHO.

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/02/askari-waaswa-kuepuka-vitendo.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa