Deputy Minister of Lands and Human Settlement Development, Hon.Angelina Mabula has ordered Local Government Authorities in Simiyu Region to use their Experts in Surveying land, so that citizens can get access to copyright of their areas and reduce land conflicts.
Mhe.Mabula ameyasema hayo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu iliyokuwa na lengo la kukagua jengo litakalotumika kama Ofisi ya Kanda ya Ardhi ya Simiyu na kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyotoa wakati wa ziara yake mwezi Agosti mwaka jana Mjini Bariadi.
Amesema ikiwa kuna Halmashauri inahitaji kupima viwanja na mashamba na ina watumishi wachache katika Idara ya Ardhi ufanyike utaratibu wa kuomba watumishi kutoka katika halmashauri nyingine ili waweze kuungana na kuweka kambi katika Halmashauri husika wafanye kazi ya kuwahudumia wananchi wengi kwa wakati mmoja.
“ Hatuna wataalam wa kutosha kuweza kupima viwanja vingi kwa wakati mmoja katika Halmashauri, lakini tunao wataalam katika Mkoa husika ambao tulishasema kama kuna uhitaji wa kupima maeneo katika Halmashauri moja wataalam wote ndani ya mkoa wakusanywe waweke kambi hapo mpaka hiyo kazi iishe , wakimaliza wanahamia wilaya nyingine” alisisitiza Mabula.
Ameongeza kuwa Halmashauri yoyote itakapoona ina uhitaji wa watalaam kutoka Ofisi ya Kanda kwa ajili ya kuongeza nguvu katika zoezi la upimaji, Ofisi hiyo ipo tayari kufanya kazi na Halmashauri yoyote itakayoomba.
Aidha, amezitaka Halmashauri mkoani Simiyu kupima maeneo yote ya Mjini pamoja na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na uwekezaji.
Kwa upande wake Kaimu Kamishna wa Kanda ya Ardhi ya Simiyu, Ndg. Makwasa Biswalo ametoa wito kwa Watalaam mkoani humo kuona namna ya kutenga eneo la mipango miji katika eneo lililopitiwa na barabara ya lami ya kilomita 70 kutoka Bariadi mpaka Lamadi(kilomita kadhaa kwenye kila upande wa barabara) ambalo ni eneo zuri kwa ajili ya uwekezaji.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema ameshazungumza na Watendaji wa Halmashauri zinazopitiwa na barabara hiyo ya Bariadi-Lamadi(KM 70) kuwa, waone namna Halmashauri hizo zinavyoweza kumiliki maeneo hayo walau kilomita moja kushoto na kulia kwa barabara hiyo.
KUPATA PICHA ZAIDI KWA AJILI YA TUKIO HILI BOFYA HAPA:- https://simiyuregion.blogspot.com/2018/01/naibu-waziri-halmashauri-zitumie.html
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa