• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Mamia ya Waombolezaji Wajitokeza Kumzika Mtoto wa Mkuu wa Majeshi

Posted on: September 27th, 2019

Mamia ya wananchi kutoka mikoa ya Simiyu, Mara, Shinyanga, Mwanza na Dar es Salaam wameshiriki katika mazishi ya mtoto wa Mkuu wa Majeshi  marehemu Nelson Mabeyo aliyekuwa rubani wa ndege ya Shirika la Auric Air, ambaye alifariki Septemba 23, 2019 kwa ajali ya ndege iliyotokea katika Uwanja mdogo wa Seronera  uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara.

Mazishi hayo yamefanyika Septemba 26, 2019 katika Kijiji cha Masanzakona wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, ambapo yalitanguliwa na ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yuda Tadei lililipo kijijini hapo ambapo ni nyumbani kwao na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo.

Akihubiri wakati wa ibada ya mazishi, Askofu Michael Msonganzila, Jimbo Katoliki Musoma amewasihi waombolezaji wote kuendelea kuifariji na kuiombea familia ya Mkuu wa Majeshi ili wapokee msiba huo kwa jicho la imani, masikio ya imani na kama mpango wa Mungu.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akitoa salamu za serikali  amesema “marehemu Nelson Mabeyo alikuwa  kijana mcheshi na mchapakazi leo hatuko naye tena nitoe pole kwa familia ya Jenerali Mabeyo, sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea niwaombe tuendelee kuwaombea katika kipindi hiki kigumu Mwenyezi Mungu awape ustahimilivu.”

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza  kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Simiyu na wakuu wa mikoa ametoa pole kwa familia ya Mkuu wa Majeshi na kumshukuru kwa namna Mkuu  alivyowaunganisha watu wa Masanza, Busega na Simiyu katika masuala mbalimbali ya  ikiwemo Ujenzi wa Kanisa ambalo ibada ya mazishi ya marehemu Nelson imefanyika.

Kwa upande wake  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenrali Venance Mabeyo amewashukuru watu wote walioshirikiana na familia yake tangu msiba wa mwanaye Nelson ulipotokea , ambapo amesema kama familia hawauchukulii msiba huo kama adhabu bali makusudi ya Mungu mwenyewe kwa mtoto wao .

Mazishi ya marehemu  Nelson Mabeyo yalihudhuriwa na  watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, viongozi na Maafisa wa JWTZ walioko kazini na wastaafu, mawaziri na manaibu waziri, makatibu wakuu, wakuu wa Taasisi, viongozi wa Vyombo vya Usalama, wabunge, Wakuu wa mikoa ya Simiyu, Mara, Shinyanga, Kagera, Kigoma, Mwanza na Dar es salaam , kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Simiyu na wakuu wa wilaya.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-http://simiyuregion.blogspot.com/2019/09/mamia-ya-waombolezaji-wajitokeza.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Karibu Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu July 04, 2022
  • " Tuna zoezi la Senza Mbele yetuni tarehe 23 Agosti 2022 Binafsi nipo tayari kuhesabiwa, nawe ukihesabiwa, wore tutakuwa tumehesaniwa na mipango endelevu itapangwa Kwa ajili yeti. Sensa Kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa" Mhe. David Kafulila July 08, 2022
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Fungua

Habari Mpya

  • DKT. YAHAYA ESMAIL NAWANDA MKUU WA MKOA MPYA SIMIYU

    July 28, 2022
  • RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA "MCHOMOKO"

    July 13, 2022
  • WANAOWAKOPA WAKULIMA WA PAMBA KUKIONA-RC KAFULILA.

    July 09, 2022
  • Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Simiyu

    July 06, 2022
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa