Saturday 28th, May 2022
@BUSEGA SIMIYU
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila wakati wa Ziara yake Wilayani Busega, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na Wavuvi wa Nyashimo,
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe.Tano Mwera aliwafahamisha wakazi wa Nyashimo kuwa ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa Mpya wa Simiyu, imelenga kusikiliza kero zao na hatimae kupata ufumbuzi wa kero hizo.Mhe.Tano aliwataka wawakilishi wa wavuvi hao kuwasilisha kero wanazokabiliana nazo katika shughuli za uvuvi, nao walikuwa na haya ya kusema;
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamikoma- Bw.Kurwa Bula;
# Changamoto, kubwa ni upumzikaji wa siku 10 hii ni changamoto kwani sisi tukipumzisha ziwa watukutoka maeneo mengine wana kuja kuvua kwetu kwani wao huwa hawapumzishi Ziwa, ni bora, basi hiyo sheria iwekwe kwa mikoa yote mitatu.Kama kufungwa kufungwe Wilaya zote za mikoa jirani
Diwani wa Kata ya Kabita- Silas Soshola
Changamoto kubwa tunazokalinana nazo ni pamoja na :
# Sheria za uvuvi, nyingi ya sheria hizo ni za zamani na si rafiki, sasa hivi tunalipa Tsh. 400,000/-, bado kuna kodi nyingi Sana,
# Wavuvi wetu tuna Walipia leseni, tunaomba hiyo leseni ifutwe kwani mbona wakulima hawalipi leseni hizo,
# Tunahitaji Masoko, tunaomba tupate masoko angalau mawili
# Tuna Shule moja tu ya Sekondari, ambayo ina Wanafunzi 1250 na waalimu 2 wa somo la Biology, Waalimu 2 -Kiswahili , waalimu 2-basic math, hatuna mwalimu wa fizikia. Wengi wa Waalimu wanaokuja hawakai.
# Wakazi wa Nyashimo walioamua kujenga shule ya Sekondari Venance Mabesho, ambapo tupo katika hatua za mwisho,tunaomba tupate angalau Mifuko 200 ya cementi kwani itasaidia sana katika ujenzi wa Uzio ili watoto wetu wasiliwe na wanyama
# Tunaomba tuwekewe alama ya Pundamilia kwani Barabara yetu inakaosa alama hiyo na kwa kipindi cha kwa miaka watu wengi wamepoteza maisha.
Wadau wengine walikuwa na haya ya kusema;
Paulo Makongoro- Mwenyekiti wa Kijiji:
Changamoto:
# Viboko, Changamoto ya viboko ambao wana angamiza watu
Marko Shonokwa:
# Tunahitaji kituo cha Polisi, Kwani na kituo cha Polisi kilichojengwa na wananchi kukamilika bado wananchi wanaenda Nyamikoma
# Kero nyingine ni ya watu kuchukua mamlaka kumtoa mtu madarakani
Semeni:
# Leseni ni kwetu tu sisi tukienda kwingine tunakamwatwa kwa nini wao wakija huku hawakamatwi
#Changamoto ya shamba la Kijiji ambalo limechukuliwa na watu ilikuwa,
Akijibu hoja hizo Mhe. Mkuu wa Mkoa alikuwa na haya ya kusema:
# Eneo la Nyashimo wilaya ya Busega lina ukanda wenye ukubwa wa kilometa za mraba 200 ambazo zinafaa kutumika kwa shughuli ya uvuvi, Uvuvi wa kutumia vizimba mbao ndio wenye tija zaidi tunavyo Vizimba 12,na kwa ujumla mnavuna tani 54,
Kwa eneo hilo linaweza Kutengeneza Vizimba zaidi ya 55,000 na kupata Samaki kiasi cha tani 250,000, na hivyo kuwa vinara katika eneo la uvuvi katika nchi hii,
#Njia nyepesi ya kupata msaada ni kukaa katika vikundi na hivyo kuirahisishia Serikali kutoa msaada mkiwa katika vikundi.
# Kuhusu suala la kodi na ushuru, Mkurugenzi na watu wako anadaeni taarifa kamili ya aina mbalimbali za ushuru au tozo.
# Pongezi kwa ujenzi wa Shule, mahitaji yenu ni shule nne na mnayo moja, hatua madhubuti zitachukuliwa ili kuona ni kwa jinsi gani tutatatua changamoto hiyo.
IMEANDALIWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA SIMIYU
Bariadi - Somanda
Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.
Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054
Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054
Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz
Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa