• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Zaidi ya Watu 300 Kushiriki Mashindano ya Baiskeli, Mbio Fupi na Ngoma za Asili Simiyu

Posted on: November 26th, 2020

Zaidi ya wanamichezo 300 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wanatarajia kushiriki Tamasha la Simiyu Jambo Festival ambalo litahusisha mashindano ya mbio za baiskeli, ngoma za asili(wagika na wagalu), mbio fupi (kilometa kumi) pamoja na mashindano ya kitaaluma kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival Bi. Zena Mchujuko wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bariadi  leo Novemba 26, 2020 juu ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 28, 2020 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

“Zawadi zitatolewa kwa mshindi wa kwanza mpaka wa kumi wanawake na wanaume (mbio za baiskeli), walemavu zitatolewa kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tano; mbio fupi tutatoa kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu,” alisema Bibi. Mchujuko.

Afisa Miradi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) ambalo ndiyo mdhamini Mkuu wa Simiyu Jambo Festival,  Bw. Dennis Swai amesema shirika hilo limeamua kudhamini tamasha hilo kwa kuwa ni fursa mojawapo ya kuiweza jamii kutambua haki za watoto wa kike na wanawake katika kufikia malengo yao,  huku akiahidi kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali kama wadau wa maendeleo.

Kaimu Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Simiyu, Bw. Mbezi Ally amesema chama hicho kimeandaa washiriki ambao ni wazuri katika mbio,  ambapo amebainisha kuwa baadhi yao wameshiriki mbio ndefu (kilomita 21 na Kilomita 42) ikiwemo Serengeti Safari Marathon na kutoa wito kwa washiriki kutoka maeneo yote ndani na nje ya mkoa kushiriki mashindano haya.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Mbio za Baiskeli Mkoa wa Simiyu, Bw. Buyaga George amesema pamoja na washiriki kutoka mkoa wa Simiyu, washiriki kutoka mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Tabora na Arusha wamethibitisha kushiriki mashindano ya mbio za baiskeli kwa wanaume (Kilomita 140) ,wanawake (kilomita 80) na walemavu (kilomita tano).

Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga amesema mkoa wa Simiyu ni maarufu kwa kutumia baiskeli kama nyenzo ya usafiri hivyo mkoa umeona haja ya kuwaendeleza wana Simiyu kwa utamaduni wao wa kutumia baiskeli ili waitumie fursa hiyo kuingia katika mashindano yanayoweza kuwafanya wawe waendeshaji bora wa baiskeli.

Aidha, Mmbaga ametoa wito kwa wadau na wafanyabiashara mkoani hapa kushiriki katika tamasha hili kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulitumia kutangaza huduma na bidhaa zinazopatikana Simiyu.

Tamasha hili la Simiyu Festival linafanyika kwa mara ya tatu sasa likiwa na Kauli Mbiu, “WAWEZESHE WANAWAKE NA WATOTO WA KIKE ILI KUWA NA DUNIA BORA” chini ya udhamini wa UNFPA, Jambo Food Products, Alliance Ginnery Ltd, Busega Mazao na SweetDreams Hotel,  Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/11/zaidi-ya-watu-300-kushiriki-mashindano.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa