• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Waziri Mbarawa Aitaka TBA Kukamilisha Miradi kwa Wakati

Posted on: February 17th, 2018

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amemtaka Wakala wa Majengo  hapa nchini (TBA), kuhakikisha anakamilisha kwa wakati  ujenzi wa miradi mbalimbali anayotekeleza

Waziri Mbarawa ameyasema hayo wakati akikagua Ujenzi wa Hospitali  ya Mkoa, Nyumba za Viongozi wa Mkoa zinazojengwa na Wakala huyo eneo la Nyaumata mjini Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani  Simiyu.

Amesema kuwa TBA ni Taasisi ya Serikali ambayo imeaminiwa na Serikali kwa kuwa  inafanya kazi vizuri lakini imekuwa ikichelewa kukamilisha miradi inayopewa  tofauti na muda uliowekwa kulingana na mikataba.

“TBA ni Taasisi ya Serikali na katika Serikali hii ya awamu ya tano tumeipa miradi mingi tukiamini kuwa watafanya kazi nzuri zenye ubora na kukamilika kwa wakati, ubora upo lakini tatizo kubwa ni kutomaliza kazi kwa wakati” alisema Waziri Mbarawa.

“TBA mjipange mhakikishe mnamaliza miradi kwa wakati vinginevyo hatutawapa kazi kwa sababu hatuwezi kuwapa fedha za Serikali jengo la mwaka mmoja mnajenga miaka mitano, naamini mkijipanga vizuri uwezo mnao na Serikali inawaamini” alisema Mbarawa.

Naye  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka pia ametoa wito kwa Wakala wa majengo TBA kukamilisha ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Mkoa huo ili viongozi waweze kupata makazi .

Wakati huo huo Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amesema kuwa ameshalipa fedha kwa TBA ili waweze kukamilisha ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Mkoa na wameahidi kukamilisha na kukabidhi nyumba hizo mwezi Mei mwaka huu.

Awali akitoa maelezo ya Miradi inayotekelezwa na TBA mkoani Simiyu, Meneja wa TBA mkoani humo Mhandisi.Likimaitare Naunga  amesema wanashindwa kukamilisha baadhi ya miradi kwa wakati kutokana na kucheleweshewa fedha.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/02/waziri-mbarawa-aitaka-tba-kukamilisha.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa