• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Wananchi 2228 Wilayani Itilima kupata Maji Safi na Salama

Posted on: July 5th, 2017

Jumla ya wakazi 2228 wa mji wa  Lagangabilili Wilayani Itilima wanatarajia kuondokana na  adha ya kupata huduma ya  maji umbali mrefu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa chanzo cha maji ya bomba chenye uwezo wa  kutoa maji kiasi cha lita za ujazo 15000 kwa saa.

 Chanzo hicho cha maji chenye mtandao wa  mabomba ya maji ya urefu wa mita 29,431 na vituo vya kuchotea 20 vitawasaidia wananchi hao kupunguza muda  waliokuwa wakiupoteza kufuata huduma ya maji umbali wa kilometa zaidi ya mbili

 Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo wa maji kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Amour Hamad Amour,mhandisi wa maji wa Halmashauri ya Itilima Goodluck  Masige amesema kuwa wananchi wa mji wa lagangabilili  wamekuwa wakifuata  maji kwa umbali  mrefu hali inayopelekea kupoteza muda mwingi ambao wangetumia  kutekeleza shughuli za maendeleo.

Masige amesema kuwa mradi huo ambao utagharimu jumla ya shilingi milioni 978 hadi kukamilika kwake utasaidia  kupunguza tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi, ambapo amesema pamoja na kuwaduhumia wananchi utaweza kutoa huduma ya maji kwa taasisi mbalimbali katika Mji wa Lagangabilili  na kunywesha mifugo.
 
 Aidha kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour amesema amefurahishwa sana na mradi huo ambao utawatua ndoo vichwani akinamama na kuwapumzisha mzigo mzito waliokuwa wakiubeba kwa kipindi kirefu.

 "Nimefurahishwa sana na mradi huu...ni  mradi ambao utakuwa na manufaa makubwa katika ustawi wa maendeleo ya wananchi sambamba na kuwatua akinamama hawa ndoo kichwani,jambo  ambalo ni azma ya Serikali ya awamu ya Tano  “ amesema

Aidha,  kiongozi huyo amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima kuunda kamati za watumia maji ili kuboresha huduma za utoaji maji kwa wananchi wote bila kujali tofauti za kiitikadi, dini ,rangi siasa wala kabila na kusimamia utunzaji wa miradi yote ya maji.

Sambamba na hilo Ndg.Amour Hamad Amour akiweka jiwe la Msingi katika jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima amepongeza Wakala wa Majengo wa Taifa(TBA) kwa kujenga jengo kubwa lenye vyumba zaidi ya 40 katika ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.

Ndg.Amour amesema jengo hilo litakapokamilika watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima walitumie vizuri kwa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa uadilifu na kuacha mazoea katika utendaji.

Pamoja na kuweka jiwe la Msingi katika Chanzo cha Mradi wa Maji Lagangabilili na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya, Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Itilima umezindua vyumba vinne vya madarasa na klabu ya wapinga rushwa shule ya sekondari Budalabujiga,kuweka jiwe msingi Bweni la Wavulana Kanadi Sekondari na kuona maboresho ya viwanda na utunzaji wa mazingira kwa ufugaji wa nyuki.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa