• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Viongozi Watakiwa Kuwakumbusha Wazazi Kuchangia Chakula Shuleni Na Kununua Sare Za Watoto Wao

Posted on: August 18th, 2018

Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wametakiwa kuwakumbusha wazazi na walezi kuwanunulia watoto wao sare za shule na kuchangia chakula mashuleni ili watoto wao waweze kusoma kwa utuivu na umakini wanapokuwa shuleni  na  kuzuia utoro .

Rai hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru baina ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera yaliyofanyika katika Kijiji cha Mkula wilayani humo.

Kabeho amesema Serikali ya awamu ya tano imefuta ada na michango mbalimbali iliyokuwa kero kwa wananchi ili kila mtoto wa Kitanzania apate haki ya Elimu kuanzia darasa la awali mpaka Kidato cha nne bila malipo , hivyo wazazi na walezi wanapaswa kuwanunulia watoto wao sare za shule pamoja na mahitaji yao mengine ya shule ikiwa ni pamoja na daftari na kalamu.

“ Kwa sasa wazazi hamlipi tena ada wala michango  wajibu wenu ni kununua sare za shule na kununua mahitaji mengine kama kalamu, daftari na mabegi ,Serikali inaendelea kuhamasisha mtimize wajibu wenu, lakini pia namuomba Mkurugenzi awaeleze Walimu wakuu sare za Halmashauri yake ni zipi ili nao wawakumbushe wazazi kwanunulia watoto wao sare hizo” alisema.

Aidha, Kabeho amesema ni vema  wazazi  na walezi wakachangia chakula shuleni ili kuwafanya wanafunzi waweze kusoma kwa utuivu na umakini wanapokuwa shuleni  na  kuzuia utoro .

“Tunaomba pia mtimize wajibu wenu kuchangia chakula shuleni kwa sababu unapotoa chakula shuleni tunapunguza utoro , tunaongeza umakini na ufuatiliaji kwa wanafunzi pale wanapofundishwa, wanafunzi wengi wao wanatoroka pale wanapohisi njaa na wakiondoka baadhi yao hawarudi” alisema Kabeho.

Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Busega na kupitia miradi saba yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 900 katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu na Viwanda.

Akizungumza mara baada ya kufungua vyumba vitatu vya madarasa na matundu matano ya vyoo katika Shule ya Sekondari Nasa, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ambayo itasaidia kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Akizungumza na Wananchi baada ya kufungua Wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Nasa Kabeho amewashukuru wananchi kwa namna wanavyojitolea nguvu kazi katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo katika Kituo hicho cha Afya cha Nasa.

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Wodi hiyo ya wazazi, Katibu wa Afya Wilaya wa Wilaya ya Busega Huruma Temu amesema kuwa wodi hiyo katika kituo cha Afya Nassa hadi kukamilika kwake imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 109 ikiwa ni fedha za wafadhili kutoka UNFPA.

Haruna alibainisha kuwa lengo kuu la kujenga wodi hiyo ya wazazi ni kuboresha afya ya uzazi na kupunguza idadi ya vifo vya akinamama na watoto Wilayani Busega.

MWISHO

 KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSUHABARI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/08/viongozi-watakiwa-kuwakumbusha-wazazi.html

 

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa