• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

TARURA Simiyu Kufungua Barabara Zilizoathiriwa na Mvua Kuzifanya Zipitike Wakati Wote

Posted on: May 13th, 2020

Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Eng. Philemon Msomba amesema Serikali imedhamiria kufungua barabara zote zilizoharibiwa na mvua mkoani hapa na kuhakikisha zinapitika kwa mwaka mzima ili kuwarahisisha wananchi  mawasiliano na usafirishaji wa bidhaa na mazao mbalimbali.

Dkt. Msomba ameyasema hayo Mei 13, 2020 wakati wa ziara yake ya kukagau maendeleo ya ujenzi wa madaraja katika wilaya ya Bariadi eneo la Mto  Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida litakalogharimu shilingi milioni 33 na daraja la Mto Nyambuli linalounganisha kijiji cha Mwamondi na Lulai (Dutwa) litakalogharimu kiasi cha shilingi milioni 25 yanayojengwa kwa mpango wa dharura.

“Azma ya Serikali ni kuhakikisha barabara zote zinapitika kwa mwaka mzima, tunaishukuru Serikali imetoa fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara mkoani Simiyu, mwaka wa fedha 2019/2020 tulitenga bajeti ya shilingi bilioni tano, kufikia Mei 13, 2020 tumepokea shilingi bilioni 4.23 sawa na asilimia 84; kwa hiyo barabara zote zilizoathiriwa na mvua tuna uhakika wa kuzifungua,” alisema Mratibu wa TARURA Simiyu, Dkt. Eng. Philemon Msomba.

Aidha, Dkt. Msomba amesema TARURA itafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa miradi yote  ikiwemo ya dhararua inatekelezwa kwa kiwango na kwa wakati ili barabara hizo ziweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi ambapo amebainisha kuwa TARURA Simiyu imeomba kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali kwa mpango wa dharura.

Dkt. Msomba amesema pamoja na ujenzi wa madaraja katika mwaka wa fedha 2019/2020  TARURA imejipanga kutengeneza mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 690 huku akiwataka Mameneja wa TARURA wa wilaya kusimamia ubora wa kazi katika ujenzi huo na kuhakikisha kazi zote zinakamilika kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewashukuru viongozi wa TARURA kwa namna walivyochukua hatua madhubuti kuhakikisha madaraja yanatengenezwa na barabara za vijijini zinapitika hususani kwenye kipindi cha mvua nyingi, huku akitoa rai kwa viongozi hao kuwasimamia wakandarasi ili wafanye kazi kwa kuzingatia viwango vya kitaalam na thamani ya fedha.

Naye Diwani wa Kata ya Dutwa, Mhe.Mapolu Mkingwa amesema matengenezo ya daraja la Mto Nyambuli linalounganisha kijiji cha Mwamondi na Lulai utaondoa adha iliyokuwa ikiwapata wananchi kufika makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Dutwa na kurahisisha usafirishaji wa mazao kwa kuwa Mwamondi ndiyo ghala la chakula kwa kata hiyo.

Wakizungumzia ujenzi wa madaraja yaliyokuwa yamesombwa na maji kutokana na mvua wananchi wa Mtaa wa Bunamhala na Majahida katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Kulwa Nyanza, Lazaro Samwel na Magreth Magile wamesema baada ya daraja kukatika iliwalazimu kutumia usafiri wa pikipiki na baiskeli  kutokana na eneo la mto Ndoba kutopitika kwa magari.

“Tulikuwa tunapata shida kuvuka mto huu na mvua zinaponyesha tulikuwa tunalazimika kutengeneza daraja la miti ili litusaidie kuvuka, tunaishukuru serikali kuchukua hatua za kuanza kujenga daraja tunaomba likamilike mapema maana huku kuna wananchi wengi na vile vile kuna chuo cha maendeleo ya jamii,” alisema Lazaro Samwel.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu unahudumia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 4038.16 ambapo kati ya hizo asilimia 55 zinapitika na ziko katika hali nzuri na wastani, huku asilimia 45 ya mtandao zinahitaji matengenezo na jitihada zinafanyika ili zifanyiwe matengenezo kuhakikisha zinapitika kwa mwaka mzima.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2020/05/tarura-simiyu-kufungua-barabara.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa