• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Simiyu Yajipanga Kuiimarisha Shule ya Sekondari Bariadi kama Shule Maalum ya Michezo

Posted on: May 31st, 2018

Serikali mkoani Simiyu imesema imekusudia kuiimarisha shule ya Sekondari ya Bariadi ambayo ilitengwa kuwa Shule ya Michezo, kwa kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike na wa kiume na kuiwekea miundombinu yote muhimu, ikiwemo viwanja vya michezo yote kwa lengo la kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati alipokuwa akifunga mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA kimkoa katika viwanja vya Shule ya sekondari ya Wasichana Maswa.

"Ningehitaji tuifanye Shule ya Sekondari Bariadi kuwa shule maalum ya kimichezo ya Kimkoa, yenye mabweni ya wavulana na wasichana na tuiwekee miundombinu yote ya michezo ili watoto wote wenye vipaji vya michezo waende pale na nitaomba kibali walimu wa michezo wahamie hapo, tufike mahali ambapo Bariadi Sekondari itatoa wachezaji wa kutumainiwa kwenye Taifa" amesema Mtaka.

Aidha, amewataka wanafunzi wote kuwa na mtazamo tofauti katika michezo kwa kuondokana na nadharia ya kuwa michezo ni afya, burudani na kwenda kwenye dhana ya michezo kama taaluma, ajira na biashara, ambapo amehimiza kuwa mkoa huo unafanya uwekezaji na mapinduzi ya michezo kibiashara katika Shule hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa pia amewataka wanafunzi hao kuuwakilisha vema mkoa na kuwatakia heri na ushindi katika mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa yatakayofanyika jijini Mwanza, huku akiwataka kuwa na nidhamu kipindi chote watakachokuwa huko na akaahidi kutoa zawadi mbalimbali kwa washiriki wote watakaporudi na ushindi.

Katika hatua nyingine Mtaka akiwakabidhi walimu na wanafunzi jezi zilizotolewa kwa udhamini wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, kupitia mradi wake wa Kiwanda cha Chaki (MASWA CHALKS) amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi mkoani humo kujipanga kwa ajili ya kudhamini mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA mwaka 2019 kupitia miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao ili kuendelea kuutangaza mkoa huo.

Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory amesema changamoto kubwa zilizowakabili washiriki wa mashindano hayo ni pamoja na upungufu wa viwanja katika shule za msingi na sekondari na kukosa wafadhili kutoka nje ili kuwezesha wanafunzi kukaa kambini muda mrefu kujiandaa na mashindano.

Kwa upande wao wanafunzi/ washiriki wa UMISSETA na UMITASHUMTA mkoa wa Simiyu wamemhakikishia Mkuu mkoa na wananchi kwa ujumla kuwa watarudi na ushindi katika mashindano hayo Kitaifa.

"Mwaka 2018 tumejipanga na ushindi ni lazima kwa mwaka huu sisi tunaenda Mwanza kushinda na kuchukua makombe, tunamhakikishia Mkuu wa Mkoa na wananchi wote wa Simiyu kuwa tunarudi na ushindi" Alisema Mwanaidi Khamis kutoka  Maswa.

Jumla ya washiriki 811 wa michezo mbalimbali kutoka katika Halmashauri zote Sita za Mkoa wa Simiyu wameshiriki mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa kwa mwaka 2018.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/05/simiyu-yajipanga-kuiimarisha-shule-ya.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa