• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Serikali kutoa Chupa 2,000,000 za Dawa ya Kuuwa Wadudu Wanaoshambulia Pamba Simiyu

Posted on: February 10th, 2018

Serikali imewahakikishia wakulima wa pamba Mkoani Simiyu kuwa itatoa chupa 2,000,000 za dawa ya kuuwa wadudu wanaoshambulia zao la Pamba ili kuwasaidia katika kukabiliana na wadudu hao.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe jana alipofanya ziara katika Wilaya ya Bariadi, Itilima na Maswa Mkoani Simiyu  kwa ajili ya kukagua mashamba ya pamba na kujionea changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba.

Mhandisi Mtigumwe amesema lengo la Serikali lilikuwa ni kutoa chupa za dawa 1,800,000 lakini kutokana kuongezeka kwa wakulima wa zao hilo,  Serikali kupitia Bodi ya Pamba imeamua kutoa chupa 2,000,000 .

“Awali tulipanga kusambaza chupa 1,800,000 lakini mahitaji yamekuwa makubwa, kwa hiyo tutaongeza na kufikia chupa 2,000,000 na kufikia mwishoni mwa mwezi Februari chupa 1,000,000 zitakuwa zimeshafika Simiyu” alisistiza Mhandisi Mtigumwe.

Aidha, Mtigumwe alisisitiza viongozi na wataalam wa Kilimo mkoani Simiyu kusimamia ugawaji wa dawa hizo kwa wakulima na kuhakikisha zinatumika vizuri.

Aliongeza kuwa Wizara imetoa wataalam wake wasiopungua 60 kutoka makao makuu ya Wizara, Kituo cha Utafiti cha Ukirigulu na Chuo cha Kilimo Ukirigulu na kuwapeleka katika mikoa yote inayolima pamba, lengo likiwa ni kutoa elimu kwa wakulima na Maafisa Ugani juu ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu(viuadudu).

Masanja Mabula mkulima wa Pamba kutoka  Kijiji cha Mbiti Wilayani Bariadi alisema katika msimu wa mwaka 2017/2018 wakulima wamehamasika kulima pamba hivyo wanaomba Serikali iwasaidie wapate dawa ili wadhibiti wadudu waharibifu.

Awali akiwasilisha taarifa ya Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini alisema Mkoa huo unahitaji chupa za dawa 1,810,839 kwa ajili ya wakulima wa pamba 309,511 ambao wamelima ekari 602,409 zikitarajiwa kuzalisha tani 421,686.3 za pamba kwa wastani wa kilo 700 kwa ekari moja.

Hadi kufikia Januari 31, 2018  Mkoa wa Simiyu umelima jumla ya hekta 241,445.2 sawa na ekari 603,613, ambazo ni asilimia 85.1 ya lengo la kulima ekari 709,296.5.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/02/serikali-kutoa-chupa-2000000-za-dawa-ya.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa