• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

NSSF yakabidhi Hundi ya Shilingi Bilioni 1.5 Upanuzi wa Kiwanda Cha Chaki Simiyu

Posted on: June 24th, 2017

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekabidhi hundi ya shilingi bilioni 1.5 kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu,  fedha ambazo ni  mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha Chaki Wilayani humo na kuongeza uzalishaji..

Hundi hiyo imekabidhiwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara amepongeza Mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza Sera ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kwa vitendo  na kuwataka viongozi wa mkoa huo kutokatishwa tamaa.

Amesema NSSF kama Shirika la Umma linatekeleza sera na maelekezo ya Serikali na wametoa mkopo huo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ili wafanye upanuzi wa kiwanda cha chaki na kuongeza uzalshaji kwa kuwa suala la Viwanda ni la kipaumbele.

Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na  watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amesema kiwanda cha Chaki Maswa kimebeba ujumbe na dhana ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya kushikamanisha Uchumi wa Viwanda na Maendeleo ya watu kwa sababu kinatumia malighafi ya hapa nchini.

Aidha, amesema kiwanda hiki kitawanufaisha Watanzania hususani vijana wa Mkoa wa Simiyu ambao watafanya kazi moja moja katika kiwanda na wale wataohusika katika uchimbaji wa malighafi ambayo inapatikana maeneo mengine  hapa nchini.

“Asilimia 56 ya nguvukazi hapa Tanzania ni vijana na vijana wengi bado hawana ajira lakini kiwanda hiki kitasaidia, kwa kuwa sehemu ya hiyo asilimia 56 wataajiriwa katika kiwanda na wengine watapata ajira huko mkoani Singida ambako malighafi ya kutengenezea chaki inapatikana” amesema.

Mhe.Mhagama ameongeza kuwa kiwanda kitatatua tatizo la upatikanaji wa chaki hapa nchini,kitaokoa fedha kwa kuwa chaki zitauzwa kwa bei nafuu na kitaongeza mapato ya fedha za kigeni kwa kuwa chaki zitakazozalishwa zitauzwa katika soko la nje ya nchi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imeonesha mfano katika kutekeleza agizo la Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli la kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa kujenga kiwanda hicho kikubwa, ambapo amesema kufikia mwaka 2020 Halmashauri za Mkoa wa Simiyu zitakuwa mfano kwa kuwa na miradi yake zenyewe .

     “Kama Halmashauri zinakopa mabilioni kujenga stendi, masoko kwa nini zisikope kujenga viwanda, zikatumia malighafi ya hapa nchini  zikaajiri Watanzania wakapata kipato na nchi yetu ikanufaika; Halmashauri za Mkoa wa Simiyu zitaajiri na kwenye miaka mitano ya Mhe.Rais tutatoa mfano wa kuwa Halmashauri zenye miradi yake” amesema.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Mhe.Riziki Pembe Juma amesema Zanzibar ni wadau wakubwa wa Chaki zinazotengenezwa Maswa(Maswa Chalks), hivyo ameomba ushirikiano ulioanzishwa kati ya Zanzibar na Simiyu udumu ili kufikia malengo katika kukuza kiwango cha elimu na utekelezaji wa Sera ya Viwanda.

Kiwanda cha kutengeneza chaki Wilayani Maswa kwa sasa kinazalisha katoni zaidi ya 180 kwa siku na chaki hizo zinatumika katika shule zilizopo katika maeneo tofauti hapa nchini,  ikiwa ni pamoja na mikoa yote za Zanzibar na baadhi ya mikoa ya Tanzania bara ikiwemo Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Geita na Tabora.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa