• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Naibu Waziri Ikupa: Kilimo si Shughuli ya Wazee

Posted on: February 25th, 2019

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe.  Stella Ikupa amewashauri Vijana nchini, kuondokana na dhana ya kuwa shughuli za kilimo ni za Wazee na badala yake watumie vitalu nyumba kujifunza kilimo chenye tija na hatimaye waweze kujikwamua kiuchumi.

Ikupa ametoa ushauri huo wilayani Maswa wakati alipowatembelea Vijana katika kitalu nyumba katika kata ya Binza  akiwa katika ziara yake wilayani humo Mkoani Simiyu Februari 25, 2019.

IKUPA amesema Vijana wanapaswa  kuachana na dhana potofu kuwa kilimo ni cha Wazee na badala yake watumie fursa za mafunzo ya kilimo na wakawe mabalozi ndani ya jamii kuwa kilimo kinaweza kuwapatia ajira na kipato.

“ Kilimo kinaweza kuwatoa vijana kutoka mahali fulani kikawapeleka mahali pengine tena wakawa na uwezo mzuri kifedha kuliko hata wale walioajiriwa katika kazi za maofisini, niwashauri vijana muione fursa kupitia vitalu nyumba ondoeni dhana kwamba eti kilimo ni kazi ya wazee si kweli” alisema.

Ameongeza kuwa vijana wanayo nafasi ya kupata mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Halmashauri zao hivyo wachangamkie fursa hiyo kupata mikopo itakayowawezesha kuendeleza shughuli zao za uzalishaji ikiwemo kilimo kupitia vitalu nyumba.

Katika hatua nyingine Mhe. Ikupa amesema ni vema Halmashauri zikazingatia masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango ya bajeti zao ili ziweze kusaidia katika utatuzi wa baadhi ya changamoto za watu wenye ulemavu.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwatumia wakalimani wa lugha ya alama ili waweze kusaidia mawasiliano kati ya walemavu wa kusikia na makundi mbalimbali ya watu ikiwemo viongozi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe amekiri kupokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Naibu Waziri Ikupa na kumhakikishia kuwa watu wenye ulemavu watalindwa, watashirikishwa katika fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa Kitalu nyumba.

Nao baadhi ya vijana wanaojihusisha na utekelzaji wa mradi wa Kitalu nyumba katika Kata ya Sola wameishukuru Serikali na kuomba ipanue wigo wa kuwafikia vijana kupitia mradi huu ili vijana wengi waweze kufikiwa mpaka ngazi ya Kata.

“ Mimi ninaishukuru Serikali yetu kwa kutuletea mradi wa kitalu nyumba, tumeshajifunza namna ya kutengeneza vitalu nyumba, kilimo bora chenye tija kupitia mradi huu, tunaomba mradi upelekwe mpaka ngazi ya kata ili vijana wengi waweze kunufaika  zaidi” alisema Rachel Paulo mkazi wa Sola Maswa.

Naibu Waziri Ikupa, anaendelea na ziara yake Mkoani Simiyu ambayo itahitimishwa tarehe 27 Februari 2019, akiwa wilayani Maswa Naibu waziri ametembelea kitalu nyumba kilichopo Sola na kunzungumza na viongozi wa Serikali na watu wenye ulemavu.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI FUNGUA KIUNGANISHI HIKI:-https://simiyuregion.blogspot.com/2019/02/naibu-waziri-ikupa-kilimo-si-shughuli.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa