• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Makamu wa Rais: Elimu ya Juu ni Nguzo Muhimu katika Kuifikia Tanzania ya Viwanda

Posted on: February 22nd, 2018

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Elimu hususani ya juu ni nguzo Muhimu ya kufikia Agenda ya Serikali ya kuwa na Tanzania ya Viwanda na kufikia Uchumi wa Kati ifikapo 2025.

Makamu wa Rais wa amesema hayo ,wakati wa akifungua kongamano la elimu ya juu na Tanzania ya viwanda lililofanyika  mjini Bariadi, lililokuwa limeandaliwa na Chuo kikuu huria Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Amesema kutokana na umuhimu huo Serikali imeamua kuwekeza katika Elimu na Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025 imeweka elimu kuwa kipaumbele cha juu kwa kuwa ndiyo kitovu cha  kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika jamii.

“Ninyi ni mashahidi kuwa Serikali imeweka mkazo kwenye elimu, tumeanza na shule za msingi, sekondari lakini pia tumeongeza bajeti kubwa kwenye mikopo ya Elimu ya Juu na tutakwenda polepole mpaka tuhakikishe Watanzania wanapata elimu ya kutosha ili kuendana na uchumi wa Viwanda” alisema.

Ameongeza kuwa  lengo kuu la ni Serikali kuongeza kipato cha wananchi kupitia viwanda ambavyo vitaongeza thamani ya mazao yanayozalishwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Aidha, amewataka washiriki wa Kongamano hilo kuja na majibu ya ni kwa  namna gani wahitimu wa Vyuo Vikuu walivyojipanga katika suala la uzalishaji viwandani na kubainisha  ikiwa fani, stadi na mafunzo waliyosomea yatakidhi mahitaji ya viwanda vinavyotakiwa kujengwa hapa nchini.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof.Elifas Bisanda amesema nchi zote zilizoendelea katika Sekta ya Viwanda zina msukumo mkubwa na udahili mkubwa wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, hivyo  upo umuhimu wa kujadili Mchango wa Elimu ya Juu katika Tanzania ya Viwanda.

Aidha, Prof.Bisanda ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu kutumia fursa ya uwepo wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa ajili ya kujiendeleza katika masomo ya elimu ya juu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amewataka waajiri wote mkoani humo kuwaruhusu watumishi kwenda kusoma kwa ajili ya kuwaandaa watumishi hao kuwa na maarifa ya kutosha.

“  Tuna shida kwenye ofisi zetu  tena wakati mwingine  ni roho mbaya tu, mtumishi anaomba kwenda kusoma Mkurugenzi anamkatalia, tukitaka nchi yetu iende mbele turuhusu watu wasome,  miaka ijayo tunataka mkoa wetu ushindane hatuwezi kushindana kama hatutawekeza kwenye maarifa” alisisitiza Mtaka.

Wasomi waliowasilisha mada mbalimbali katika Kongamo hilo la Elimu ya Juu na Tanzania ya Viwanda ni pamoja na Prof. Rwekaza Mukandala, Prof.Elifas Bisanda , Prof.Uswege Minga, Dkt. Adolf Rutayuga, Dkt. George Mgode, Balozi Nicholas Kuhanga na Mhe.Anthony Diallo.

Kongamano hili lililokuwa na Mada kuu isemayo: “Mustakabali wa Elimu ya Juu kuelekea Tanzania ya Viwanda” limehudhuriwa na wanafunzi wa shule za sekondari, walimu, Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kutoka Mwanza pamoja na viongozi wa Serikali.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI KATIKA HABARI HII FUNGUA HAPA:-https://simiyuregion.blogspot.com/2018/02/makamu-wa-rais-elimu-ya-juu-ni-nguzo.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa