• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Balozi wa Ireland, Indonesia nchini Tanzania na Mwakilishi wa UNFPA Wamuahidi Ushirikiano RC Mtaka

Posted on: February 2nd, 2018

Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock amemuahidi Mkuu wa Mkoa wa simiyu Mhe Anthony Mtaka kuendeleza ushirikiano na Mkoa wa Simiyu ili kuboresha sekta ya Afya kupitia Irish Aid.

Balozi huyo ameyasema hayo wakati wa mazungumzo ya pamoja na Mhe Mtaka ambapo tayari kwa pamoja wamekubaliana kuanza kutekelezwa wa kusudio hilo tarehe 6 Februari 2018 kwa kuanza na timu ya wataalamu kufika Mkoani humo ili kuanza haraka shughuli hiyo.

Balozi Mhe. Paul Sherlock amemuahidi Mhe Mtaka kuwa tayari nchi yake ya Ireland imekusudia kwa dhati kushirikiana vyema na Mkoa huo huku akisisitiza kuendelea kushirikiana zaidi pia katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kwenye sekta ya Mifugo, Kilimo na Utalii.

Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock ametoa kauli hiyo ya kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka za katika kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji wakati alipokutana na kufanya mazungumzo leo 2 Februari 2018 katika.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Anthony Mtaka amemshukuru Balozi Sherlock kwa ubalozi wa Ireland kukubali kuwezesha safari ya mafunzo kwa wataalamu wawili kutoka Mkoani Simiyu kwenda nchini Ireland kuanzia Februari 12 mpaka 16 Machi 2018 kwa ajili ya kupata mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hasa kwenye upande wa uhifadhi wa Data za Mkoa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu Mhe Mtaka alikutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkaazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi Jacqurline Mahon ambapo pamoja na mambo mengine Shirika hilo limetoa zaidi Bilioni 3 kwa ajili ya kukarabati vituo vya afya na upasuaji ndani ya Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu.

Pia UNFPA imeahidi kutoa magari kwa Halmashauri 6 za Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kuboresha huduma za afya, ambapo tayari UNFPA wameamua kujenga ofisi yao ndogo ndani ya Mkoa wa Simiyu itakayoratibu shughuli mbalimbali za shirika hilo kwa mikoa yote ya kanda ya ziwa.

Wakati huo huo Mhe Mtaka amekutana na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Prof Ratlan Pardede ambaye pamoja na mambo mengine amekubali kutembelea Mkoa wa Simiyu mwezi Machi mwaka huu 2018 huku akiwaalika wataalamu wa Mkoa wa Simiyu nchini Indonesia mwezi Aprili mwaka huu.

Aidha, Balozi huyo Prof Pardede alisema kuwa pia sekta rasmi ya Indonesia itazuru Mkoani Simiyu ili kuona uwezekano wa kujenga kiwanda kitakachosaidia kuongeza thamani ya zao la pamba, kuboresha mkoa dada wa Indonesia na Simiyu katika mazao ya Mpunga na pamba pamoja na kualika wawekezaji wa Indonesia kuwekeza Mkoani Simiyu kwa kuzingatia Mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa wa Mkoa huo (Simiyu Investment Guide).

Balozi Prof Pardede ameusifia Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu kwamba ni wa kipekee na alipouona mwongozo huo kupitia mtandao wa Youtube aliona ukiwa umeitangaza sana Tanzania na wafanyabiashara wa Indonesia walihamasika sana kuuona na kuusoma katika Tovuti hiyo.

MWISHO

KUPATA PICHA ZAIDI JUU YA HABARI HII FUNGUA HAPA:http://simiyuregion.blogspot.com/2018/02/balozi-wa-ireland-indonesia-nchini.html

Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • RC Simiyu Asitisha Leseni Za Uchimbaji Madini Mgodi wa Lubaga

    December 17, 2020
  • Waziri wa Kilimo Prof. Mkenda, Naibu Waziri TAMISEMI Dkt Dugange Wanogesha RCC Simiyu

    December 16, 2020
  • TANROADS Simiyu Kutumia Bilioni 11.4 Ujenzi wa Barabara na Madaraja

    December 16, 2020
  • Viongozi, Wananchi na Wadau Simiyu Watakiwa Kushirikiana Kukamilisha Ujenzi wa Madarasa

    December 13, 2020
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa