• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo |
    • Barua pepe |
Simiyu Region

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dhamira na Dira
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Health Service and SocialWelfare
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Elimu
      • Huduma za Maji
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • TEHAMA
      • Ununuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
      • Strong
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Hotuba
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari
    • Video
    • Albamu ya Picha
    • Matukio yajayo
  • Miradi
    • Miradi iliyotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
  • Wilaya na Halmashauri
    • Wilaya
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
      • Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Meatu
    • Halmashauri
      • Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
      • Halmashauri ya Mji wa Bariadi
      • Halmashauri ya Wilaya ya Busega
      • Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
      • Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
      • Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
  • Uwekezaji na Utalii
    • Fursa za Uwekezaji
    • Wanyamapori na Utalii

Baada ya Kiwanda cha Chaki Simiyu Yajipanga Tena Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa, Ujenzi wa Kiwanda cha Nyanya na Pilipili

Posted on: September 14th, 2017

Baada ya mikakati ya upanuzi wa kiwanda cha kutengeneza chaki Wilayani Maswa, Mkoa wa Simiyu umejipanga tena kufanya upanuzi wa Kiwanda cha kusindika Maziwa kilichopo Wilayani Meatu na Ujenzi wa kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili wilayani Busega.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia zoezi la upembuzi yakinifu kwa viwanda hivyo lililofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa Ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP), kukamilika na taarifa yake kuwasilishwa kwa Viongozi na wadau wa Maendeleo Mkoani Simiyu katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.

Akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Wilayani Meatu, Profesa Lusato Kurwijila kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) amesema Tanzania inazalisha maziwa lita bilioni 2.1 kwa mwaka, lakini yanayopelekwa viwandani kusindikwa ni asilimia tatu ya maziwa yote, kutokana na ukosefu wa miundombinu ya kukusanyia maziwa.

Amesema upanuzi wa kiwanda cha Maziwa Meatu ni mradi unaotekelezeka hivyo ni vema ukafanyika uwekezaji katika ufugaji wa kisasa ili kupata maziwa ya kutosha, miundombinu ya  kukusanyia na kupozea maziwa,  kuwahamasisha wafugaji kuunda vyama vya ushirika ambavyo vitamiliki na kuendesha vituo vya kukusanyia maziwa na kutoa ajira kwa wananchi hususani vijana na wanawake.

Akizungumzia uanzishwaji wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, Mtaalam  wa Bustani  na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) Profesa Theodosy  Msogoya amesema, mradi huo unaweza kutekelezwa kwa mafanikio, hivyo ametoa wito kwa Serikali kuajiri watalaam wa Bustani na kuwahamasisha wakulima kujiunga katika vikundi ili waweze kukopesheka.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) Profesa Jeremia Makindara amesema, uwepo wa fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na utashi wa kisiasa,upatikanaji wa malighafi, nguvu kazi, maji, kiwanda kujengwa katika njia kuu ya usafirishaji (barabara ya Mwanza-Musoma), upatikanaji wa soko la uhakika kutasaidia kukiletea kiwanda hicho faida.

Kwa upande wao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya na Mkurugenzi wa Wilaya ya Meatu, Ndg. Fabian Manoza wamesema, viwanda hivyo vitakuwa vyanzo vipya vya mapato kwa Halmashauri zao na kuwasaidia wananchi kupata ajira na kukukuza uchumi wao.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa UNDP hapa nchini Ndg, Amoni Manyama ametoa wito kwa Serikali Mkoani Simiyu kuona namna ya kuwashirikisha wanufaika wa TASAF katika maendeleo ya viwanda na kuhakikisha kuwa makundi yote hususani wanawake yanashirikishwa na kunufaika na uanzishwaji wa viwanda hivyo.

 Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema watayafanyia kazi yote yaliyoanishwa katika Tafiti zilizofanywa na Watalaam hao kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA)na upembuzi yakinifu huo na kuyaweka katika matendo.

“Tumekuwa ni mkoa ambao tunawashirikisha wataalam kutoka katika vyuo vyetu, dhamira yetu ni kuona matokeo na position(Nafasi) yetu kama Mkoa ni kujipanga  kimkakati na mpango kazi wetu, dira ya mkoa na tunasema  kwenye miaka mitatu tutatekeleza” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema Serikali Mkoani humo iko tayari kushirikiana na sekta binafsi katika uwekezaji, hivyo ametoa wito kwa Watanzania walio tayari kuwekeza Mkoani humo kwa kushirikiana na Halmashauri ambazo zimeanzisha miradi hiyo ya viwanda.

Sambamba na hilo amezishukuru Taasisi za Fedha zilizo tayari kufanya kazi na Mkoa wa Simiyu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwepo mradi wa kilimo cha Umwagiliaji wilayani Busega hususani Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) ambayo imesema iko tayari kufanya kazi na Mkoa huo, katika miradi mbalimbali ya Kilimo.

Upembuzi yakinifu wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika nyanya na pilipili wilayani Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa wilayani Meatu uliofanywa na Wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii(ESRF) ulianza kufanyika Mwezi Julai mwaka huu na kukamilika mapema mwezi Septemba.

Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini Ndg.Amoni Manyama (kushoto) akizungumza na Viongozi na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) uliofadhili na shirika hilo.

Mtaalam wa Maziwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA), Profesa Lusato Kurwijila akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.

Mtaalam wa Uchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Mutahyoba Baisi akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.

Mtaalam  wa Kilimo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) Profesa Theodosy T. Msogoya akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.

Mhandisi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) Profesa  Benard  Chove akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.

Baadhi ya viongozi na wadau wa maendeleo Mkoani Simiyu wakifuatilia taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), iliyowasilishwa katika kikao maalum Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi na wadau wa maendeleo Mkoani Simiyu wakifuatilia taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), iliyowasilishwa katika kikao maalum Mjini Bariadi.



Matangazo

  • Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 18, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020 - Chaguo la Pili (Second Selection) January 03, 2020
  • Orodha ya Wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu waliochaguliwa Kidato cha Kwanza mwaka 2020 Shule za Serikali za Bweni na Kutwa December 07, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha NNe mwaka 2018 January 24, 2019
  • Fungua

Habari Mpya

  • Wastaafu Wawaasa Watumishi Kufanya Kazi kwa Kujituma

    April 14, 2021
  • Malalamiko ya Wachimbaji, Wenye Mashamba Mgodi wa Bulumbaka Bariadi Yashughulikiwe: RAS Simiyu

    April 08, 2021
  • Viongozi Simiyu Waaswa Kutumia Busara Badala ya Nguvu

    March 14, 2021
  • Serikali Yaanza Maandalizi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Mwanza-Isaka, Bandari Kavu Kujengwa Simiyu

    March 09, 2021
  • Fungua

Video

Upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji kupitia Teknolojia ya Ndege Nyuki (Drones)
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa(Fursa za Uwekezaji)
  • Historia ya Mkoa
  • Takwimu za haraka
  • Picha za Matukio Mbalimbali
  • Vivutio vya Utalii

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Serikali
  • Watumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bariadi - Somanda

    Anuani ya Posta: S. L. P. 4, BARIADI.

    Simu ya Mezani: 028-2700011/2700054

    Simu ya Mkononi: 028-2700011/2700054

    Barua Pepe: ras@simiyu.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo
    • Ramani

Hati Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.Haki Zote Zimehifadhiwa